Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isha afichua mchango wa marehemu Dida

DIDA Pict

Muktasari:

  • Katika kuadhimisha miaka 20 ya muziki wake, Isha ametumia fursa hiyo kutambua nafasi ya watu waliomsaidia kufika alipo, akionyesha kuwa safari ya msanii haitegemei kipaji pekee, bali pia ushirikiano na mchango wa watu wengine.

MWIMBAJI wa Taarab, Isha Mashauzi, amemtaja marehemu Khadija Shaibu, maarufu Dida, kuwa miongoni mwa watu waliochangia kukuza muziki wa Taarab nchini kupitia vyombo vya habari na kuutambulisha kwa mashabiki.

Isha amesema safari yake ya muziki haiwezi kutenganishwa na mchango wa watu waliomuunga mkono katika hatua mbalimbali, wakiwamo wanamuziki na watangazaji walioitangaza kazi yake na kusaidia muziki wa Taarab kuwafikia watu wengi zaidi.

Miongoni mwa aliowakumbuka ni Dida, mtangazaji aliyejipatia umaarufu kupitia vipindi vya Taarab. Dida aliwahi kufanya kazi Times FM katika kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kabla ya kujiunga na Wasafi FM, ambako aliendesha kipindi cha Mashamsham.

ISH 01

Dida alifariki dunia Oktoba 4, 2024, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mchango wa watu hao, Isha alisema: “Wamekuwa na mchango mkubwa. Tusingefika hapa, hasa marehemu Dida Shaibu, Mungu amlaze mahali pema peponi.”

Mbali na Dida, Isha pia amekuwa na historia ya kufanya kazi na Mzee Yusuf katika bendi ya Jahazi Modern Taarab kabla ya kuendelea na safari yake kupitia bendi yake ya Mashauzi Classic.

ISH 02

Uzoefu huo ni sehemu ya safari yake ndefu katika tasnia ya Taarab, ambako amejenga jina kwa miaka mingi kupitia nyimbo na maonesho mbalimbali.

Isha pia aliwakumbuka Siza Mazongela wa Segere pamoja na wazazi wake waliofariki dunia na watu wengine aliowataja kuwa na mchango katika maisha na safari yake ya kisanii.

Katika kuadhimisha miaka 20 ya muziki wake, Isha ametumia fursa hiyo kutambua nafasi ya watu waliomsaidia kufika alipo, akionyesha kuwa safari ya msanii haitegemei kipaji pekee, bali pia ushirikiano na mchango wa watu wengine.