Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bongo Fleva, Taarabu kuiteka Super Dome

MASHAUZI Pict

Muktasari:

  • Sauti ya Hip Hop kutoka kwa Fid Q, nayo inatarajiwa kusikika ikitetemesha jukwaa la Super Dome siku hiyo ili kukamilisha mchanganyiko wa ladha mbalimbali za muziki.

MALKIA wa miondoko ya Taarab nchini, Isha Mashauzi, yuko tayari kuandika ukurasa mwingine wa kihistoria katika safari yake ya muziki anapoadhimisha miaka 20 ya kuitumikia tasnia hiyo leo Oktoba 24, 2026, ndani ya Ukumbi wa Super Dome, Masaki, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, staa huyo amewatoa hofu mashabiki wake na kuweka wazi kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamefikia hatua za mwisho, huku akiahidi mambo makubwa yatakayofanya usiku huo kuwa wa kipekee.

“Maandalizi hadi sasa yameshakamilika kwa asilimia 97, tunamalizia vitu vidogo tu. Mashabiki wangu wakae tayari kwa sababu kutakuwa na sapraizi kibao ambazo sijawahi kuzifanya miaka yote 20 ya muziki wangu,” anasema Isha Mashauzi.

MASHA 01

Shoo hiyo itapambwa na wanamuziki wengi wakiwemo Khadija Kopa, Ben pol, G Nako, Fid Q ambapo wamezungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti kuhusu shoo hiyo.

Akizungumzia uhusiano wake na Isha na uwezo wa mwanamuziki huyo, Khadija Kopa anasema anamfahamu tangu akiwa mdogo na anatambua kipaji chake cha kuimba.

“Isha ni mwanangu na ni msanii aliyepambana hadi kufika hapa. Siku hiyo ya tarehe 24 nitakuwepo Super Dome kumshika mkono na kuwapa mashabiki burudani ya hatari ambayo hawataisahau,” anasema Khadija.

MASHA 02

Mkali wa miondoko ya R&B nchini, Ben Pol, pia anatarajiwa kupanda jukwaani na kuongeza ladha ya kipekee kwenye tamasha hilo kubwa la miaka 20.

Ben Pol amesema ni heshima kusherehekea miaka 20 ya mwanamuziki Isha Mashauzi. Siku hiyo nitahakikisha mashabiki wa Bongo Fleva na Taarab wanapata burudani ya kiwango cha juu kabisa.”

Sauti ya Hip Hop kutoka kwa Fid Q, nayo inatarajiwa kusikika ikitetemesha jukwaa la Super Dome siku hiyo ili kukamilisha mchanganyiko wa ladha mbalimbali za muziki.