Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isha Mashauzi afichua siri ya ‘Nani Kama Mama’

ISHA Pict

Muktasari:

  • Isha amesema wimbo huo ulitokana na tukio binafsi maishani mwake, lililomfanya aamue kutumia kipaji chake cha muziki kufikisha ujumbe wa kuomba radhi kwa mama yake.

MWIMBAJI wa Taarab, Isha Mashauzi, amefichua historia ya wimbo wake Nani Kama Mama, akieleza kuwa aliutunga kwa lengo la kumuomba msamaha mama yake mzazi, Bi Rukia Juma, baada ya kumkosea.

Isha amesema wimbo huo ulitokana na tukio binafsi maishani mwake, lililomfanya aamue kutumia kipaji chake cha muziki kufikisha ujumbe wa kuomba radhi kwa mama yake.

Akieleza kilichomsukuma kuutunga wimbo huo, Isha alisema: “Kwa nini? Kwa sababu ina historia kwenye maisha yangu. Niliwahi kumkera mama, nikamuomba radhi kwa kupitia ‘Nani Kama Mama’.”

ISH 01

Kauli hiyo inaonyesha kuwa wimbo huo ulikuwa na maana ya kipekee kwake, kwani haukuwa kazi ya muziki pekee, bali pia njia ya kueleza hisia zake na kuomba msamaha kwa mtu aliyekuwa na nafasi muhimu katika maisha yake.

Mama yake Isha, Bi Rukia Juma, pia alikuwa sehemu ya tasnia ya Taarab, ambako aliwahi kufanya kazi na bendi za T.O.T na Mashauzi Classic. Hata hivyo, Bi Rukia alifariki dunia mwaka 2019.

Historia ya wimbo huo inatoa taswira ya uhusiano wa Isha na mama yake, huku ikionyesha namna alivyotumia muziki kuwasilisha ujumbe wake wa kuomba msamaha wakati mama yake akiwa hai.

ISH 02

Katika safari yake ya miaka 20 ya muziki, Isha ameendelea kujijengea jina kupitia nyimbo zake za Taarab. Hata hivyo, simulizi ya Nani Kama Mama imeweka wazi upande mwingine wa maisha yake, ikieleza namna tukio binafsi lilivyogeuka kuwa sehemu ya kazi yake ya muziki.