Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize adakwa na Polisi Kenya

Harmonize adakwa na Polisi Kenya

Muktasari:

  • Kukamatwa kwake kulijiri saa chache baada ya kumaliza kutumbuiza kwenye tamasha katika KICC jijini Nairobi.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ anashikiliwa na polisi nchi Kenya kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya uongo.

Msanii huyo anashikiliwa katika kituo cha polisi Kileleshwa nchini humo.

Vyanzo vya habari kuhusu tukio hilo vinasema kuwa msanii huyo alikamatwa akidaiwa kukosa kuonekana katika vilabu kadhaa jijini Nairobi licha ya kupokea pesa kwa ajili ya kutumbuiza.

Kukamatwa kwake kulijiri saa chache baada ya kumaliza kutumbuiza kwenye tamasha katika KICC jijini Nairobi.

Harmonize amekuwa nchini Kenya tangu Ijumaa April 29 na alipanga kurudi Tanzania leo Jumapili Mei 1.