Dolly Parton afariki dunia akiwa na miaka 80
Muktasari:
- Kifo cha mwimbaji huyo maarufu kimethibitishwa jioni hii kupitia video iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram na mpwa wake, Bryan Seaver, ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa ulinzi wake.
Nguli wa muziki wa country duniani, Dolly Parton amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Kifo cha mwimbaji huyo maarufu kimethibitishwa jioni hii kupitia video iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram na mpwa wake, Bryan Seaver, ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa ulinzi wake.
Seaver amesema tangazo hilo la video lilikuwa jambo ambalo Dolly alimuomba alifanye miaka kadhaa iliyopita, kabla hajalifikiria kama siku moja lingekuja kuwa la kweli.
Parton, ambaye mara nyingi amekuwa akiitwa “Malkia wa Muziki wa Country”, alifanya kazi ya muziki kwa takribani miaka 60.
Mkongwe huyo anajulikana zaidi kupitia nyimbo zake maarufu kama Jolene na 9 to 5.
Kifo chake kimekuja baada ya miezi kadhaa ya changamoto za kiafya, hali iliyomfanya kujiondoa katika baadhi ya shughuli na matukio ya hadhara na kuwafanya mashabiki kuwa na wasiwasi kuhusu afya yake.
Alitoka katika familia ya watoto 12, akiwa mtoto wa nne kati ya 12 wa familia yake.
Alizaliwa Januari 19, 1946, huko Pittman Center, Tennessee, Marekani.