Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dogo Paten na radio ile ni stori kuhusu mazoea

Muktasari:

  • Tukamuuliza maswali mawili matatu mara ghafla mwandishi mwenzangu akamuuliza, “unaonaje kuhusu Zuchu”. Mimi nikashangaa kimoyokimoyo, ‘Zuchu!? Zuchu ameingiaje kwenye mahojiano na msanii huyu?’. Sikuwa peke yangu, msanii tuliyekuwa tunamuhoji naye alikuwa na swali kama hilo, akamuuliza mwandishi mwenzangu, ‘Zuchu ameingiaje kwenye mahojiano yangu?’

Siku moja mimi na mwandishi mwenzangu tulikuwa tunamuhoji msanii mkongwe wa kike wa muziki. Ilikuwa ni kwa ajili ya moja ya shoo zake za kutimiza miaka kadhaa kwenye gemu. Akaja ofisini, tukampokea, tukamtembeza kidogo aone tunavyofanya kazi kisha tukampeleka studio taa, kamera na mic zikawashwa.

Tukamuuliza maswali mawili matatu mara ghafla mwandishi mwenzangu akamuuliza, “unaonaje kuhusu Zuchu”. Mimi nikashangaa kimoyokimoyo, ‘Zuchu!? Zuchu ameingiaje kwenye mahojiano na msanii huyu?’. Sikuwa peke yangu, msanii tuliyekuwa tunamuhoji naye alikuwa na swali kama hilo, akamuuliza mwandishi mwenzangu, ‘Zuchu ameingiaje kwenye mahojiano yangu?’

Mwenzangu akawa anajaribu kulazimisha kuonyesha kwamba swali lake lilikuwa la msingi, na kadri alivyokuwa anafanya hivyo, ndivyo alivyokuwa anazidi kumkwaza msanii tuliyekuwa tunamhoji. Matokeo yake msanii akavua mic, akasimama na kusema kwaherini, akaondoka katikati ya mahojiano kwa hasira. Alibamiza mlango bado kidogo tuuokote chini.

Stori ya Dogo Paten na waandishi wa kipindi cha radio ya FM imenikumbusha mkasa wangu na mwandishi mwenzangu. Na kama huelewi kinachoendelea ni hivi, majuzi kati msanii wa singeli Dogo Paten alikwenda kwenye mahojiano na kipindi cha radio moja ya FM. Akiwa pale ni kama alipishana na waandishi na matokeo yake mahojiano yakaishia kati.

Nilikuwa nataka kusemaje -- washikaji waliokuwa wakimuhoji Dogo Paten walikuwa wanateswa na kilichokuwa kinamtesa mwandishi mwenzangu; kutojipanga, kufanya kazi kwa mazoea na mzuka. Mnajua kesho msanii anakuja, kisa mnamfahamu msanii, mnajua ngoma zake na habari zake mmezisikia sana mitandaoni na kwenye media nyingine, mnajua tu mtapata maswali katikati ya mahojiano. Ni kweli maswali mtayapata lakini je, yatakuwa maswali ya msingi?

Kwa mfano, kwenye mahojiano ya radio ile, kuna muda mwandishi anamuuliza Dogo Paten, ‘‘Vipi, huwa unazungumza na Zuchu?”, Dogo Paten anajibu, “Ene taimu.” akimaanisha wanazungumza sana tu, mwandishi anasema, ‘Mpigie hapo tumsalimie,” Dogo Paten anajibu, “Siwezi kumsumbua tajiri. Yaani nimpigie kwa sababu wewe umesema nimpigie braza. Siwezi.”

 Waandishi wanamaindi, wanasema hawakutegemea majibu kama hayo, ulitegemea majibu gani? Ulikuwa unataka kufanikisha nini kwa swali lako? Je, kuna taarifa umezisikia kwamba Zuchu na Paten hawaongei? Kama ndo unachotaka kuthibitisha kwanini usitafute namna nyingine ya kumchokonoa muhojiwa mpaka akupe unachotaka?

Kuna muda mwandishi anamuuliza Dogo Paten, ‘Vipi kuhusu shule maana uko form four wewe?’, Paten anajibu ‘Sitaki kuongelea kuhusu shule.’ Mwandishi anashangaa na kuuliza kwanini? Dogo Paten anajibu, ‘Sijaja kuongelea maisha yangu.’ 

Mwandishi anashangaa anauliza, ‘Kumbe umekuja kufanya nini?’ Paten anajibu ‘Nimekuja kuongelea muziki wangu.’  Waandishi wana-maindi. Wanasema Dogo anavimba, ana dharau wakati hajala hata Krismasi tatu mjini.

Narudia tena, ni wazi kwamba waandishi hawakujipanga na kujiandaa, walikuwa wanategemea kubebwa na uzoefu na vibe.

Licha ya kwamba uzoefu ni mzuri, lakini mzoefu aliyejipanga ni bora zaidi.