Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Davido atamba kwa nyimbo zake, atoa chalenji ya Sh2.65 bilioni

DAVIDO Pict

Muktasari:

  • Davido amesema yuko tayari kutoa dola milioni moja (Sh2.65 bilioni) kwa msanii atakayefanikiwa kutoa nyimbo zitakazozidi ubora na mafanikio ya kazi zake, hatua ambayo imeongeza hamasa miongoni mwa mashabiki na wasanii wa kizazi kipya cha Afrobeats.

MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Davido, ameibua ushindani katika muziki wa Afrobeats baada ya kujigamba kuwa ana nyimbo nyingi zilizofanya vizuri ambazo ni vigumu kuzidiwa na msanii mwingine.

Davido amesema yuko tayari kutoa dola milioni moja (Sh2.65 bilioni) kwa msanii atakayefanikiwa kutoa nyimbo zitakazozidi ubora na mafanikio ya kazi zake, hatua ambayo imeongeza hamasa miongoni mwa mashabiki na wasanii wa kizazi kipya cha Afrobeats.

Hata hivyo, hadi sasa haijaelezwa kwa uwazi namna mshindi wa changamoto hiyo atakavyopatikana, vigezo vitakavyotumika kupima mafanikio ya nyimbo hizo wala muda ambao msanii atapewa kuthibitisha uwezo wake.

Kauli hiyo imekuja wakati muziki wa Nigeria ukiendelea kuwa na ushindani mkubwa, huku nchi hiyo ikiwa imeibua wasanii wanaofanya vizuri ndani na nje ya Afrika, wakiwamo Wizkid, Burna Boy, Olamide, Tems, Tiwa Savage, Yemi Alade, Tekno na Ayra Starr.

DAVI 01

Chalenji hiyo ya Davido pia inakumbusha tukio la mwaka 2020, wakati msanii mwenzake Burna Boy alipowahi kuingia kwenye mvutano wa aina hiyo na wasanii wengine. Reekado Banks, aliyekuwa miongoni mwa wasanii waliotamba kupitia lebo ya Mavin Records, alijitokeza kukabiliana na chalenji hiyo, ingawa Burna Boy hakuliona jaribio hilo kama ushindani unaostahili.

Tofauti na wakati huo, safari hii macho ya mashabiki yameelekezwa kwa wasanii wakubwa wa kizazi cha sasa kuangalia kama kuna atakayekubali chalenji ya Davido na kujaribu kuthibitisha kuwa anaweza kutoa kazi zenye mafanikio makubwa zaidi.

Davido, aliyezaliwa Novemba 21, 1992, Atlanta nchini Marekani, alikulia Lagos, Nigeria, ambako ndipo alipojenga msingi wa safari yake ya muziki.

DAVI 02

Alianza kujihusisha zaidi na utayarishaji na kurekodi muziki akiwa bado kijana kabla ya kujijenga rasmi kama msanii.

Albamu yake ya kwanza, Omo Baba Olowo, ilitolewa mwaka 2012 kupitia HKN Music na kumsaidia kujenga jina katika muziki wa Nigeria. Baadaye aliendelea kutoa vibao mbalimbali vilivyompa umaarufu Afrika na katika soko la kimataifa.

Miongoni mwa nyimbo zake zilizofanya vizuri ni Dodo na Fall, huku Fall, iliyotoka mwaka 2017, ikiwa miongoni mwa kazi zilizomsaidia zaidi Davido kupanua jina lake kimataifa.

Katika tuzo za BET, Davido amewahi kushinda kipengele cha Best International Act: Africa, huku ushindi wake ukionyesha nafasi aliyojijengea katika muziki wa Afrika kwenye jukwaa la kimataifa.

Pamoja na mafanikio hayo, Davido amewahi kuwania tuzo za Grammy bila kufanikiwa kushinda, katika ushindani uliowakutanisha wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika kwenye tuzo hizo.

Sasa swali linalobaki ni kama kuna msanii wa Afrobeats atakayejitokeza na kukubali chalenji hiyo ya Davido.