Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Data za Harmonize akija na albamu ya sita

HERMONIZE Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Harmonize, albamu hiyo iliyopewa jina la 31, si albamu tu, bali ni taswira ya safari yake kimuziki, ukuaji wake, hisia zake na matukio yaliyomjenga hadi kuwa msanii tunayemuona leo.

STAA wa Bongofleva, Harmonize yupo katika maandalizi ya mwisho kabisa ya kuachia albamu yake ya sita ambayo inatarajiwa kusikika Septemba 4 mwaka huu baada ya kusogezwa mbele mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa Harmonize, albamu hiyo iliyopewa jina la 31, si albamu tu, bali ni taswira ya safari yake kimuziki, ukuaji wake, hisia zake na matukio yaliyomjenga hadi kuwa msanii tunayemuona leo.

"Kila kovu, kila hasara na kila ushindi vimefanya jambo hili kutokea wakati huu..." anasikika Harmonize akisema katika utambulisho (trailer) wa albamu hiyo.

Mwaka uliopita ambapo albamu hiyo ilipaswa kutoka, ndipo Harmonize alitimiza umri wa miaka 31, pengine ndio sababu ya kuipa albamu hiyo jina hilo ikiwa ni mara ya kwanza kutoa albamu yenye jina la namba.

HERMO 01

Hata hivyo, yeye si mwanamuziki wa kwanza katika Bongofleva kuwa na albamu au Extended Playlist (EP) yenye jina la namba, Lady Jaydee ana albamu inaitwa 20 (2021), na Mimi Mars ana albamu inaitwa 17 (2026).

Tukija kwenye EP, Abigail Chams ana EP inaitwa 5 (2023), na Marioo ana EP inaitwa MMMCXII (2026), namba za kirumi ambazo zinawakilisha tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 31/12.

Harmonize, mwanzilishi wa Konde Music Worldwide, anakuja na albamu hiyo ikiwa ni miaka 10 tangu alipotoka rasmi kimuziki mara baada ya kusainiwa na WCB Wasafi, lebo ambayo alifanya nayo kazi kwa miaka minne.

HERMO 02

Kwa sasa anashikilia rekodi kama msanii pekee wa Bongofleva aliyeweza kutoa albamu kwa miaka mitano mfululizo akifanya hivyo kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 ambapo ndipo aliachia albamu ya mwisho.

Albamu hizo ni Afro East (2020), High School (2021), Made For Us (2022), Visit Bongo (2023) na Muziki wa Samia (2024). Albamu hizi kwa ujumla zina nyimbo 76, zenye urefu (muda) wa dakika 246, sawa na saa nne.

Tunaweza kusema albamu yake ya nne (Visit Bongo) ndio ilifanya vizuri zaidi kwa sababu ilishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2023 kama Albamu Bora ya Mwaka baada ya kuwania kipengele hicho mara mbili mfululizo bila ushindi wowote.

HERMO 03

Ushindi huo ulikuja baada ya kuzibwaga albamu zifuatazo - 5 (Abigail Chams), Swahili Kid (D Voice), Most People Want This (Navy Kenzo) na Flowers III (Rayvanny).

Albamu yake ya pili (High School) iliwania TMA 2021 ikakosa, ilichuana na albamu nyingine kama 'Ona' ya Marco Chali, 'Live At Sauti za Busara' ya Wakazi, 'Air Weusi' ya Weusi na Only One King ya Alikiba iliyoibuka na ushindi.

Harmonize akarejea tena TMA 2022 na albamu yake ya tatu (Made For Us) ila akaangukia pua tena, awamu hii ilichuana na albamu kama 'The Kid You Know' ya Marioo, 'Street Ties' ya Conboi, 'Romantic' ya Kusah na 'Love Sounds Different' ya Barnaba iliyoshinda.

HERMO 03 (1)

Albamu zote tano za Harmonize, zimetoka chini ya usimamizi wa lebo yake ya Konde Music Worldwide ambayo alitangaza kuifungua hapo Oktoba 10, 2019, muda mfupi tangu kuachana na WCB Wasafi yake Diamond Platnumz.

Kipindi yupo WCB Wasafi, Harmonize hakutoa albamu bali EP, Afro Bongo (2019) ambayo aliwashirikisha Diamond, Yemi Alade, Mr. Eazi na Burna Boy, mshindi wa Grammy 2021 katika kipengele cha Albamu Bora Duniani.

Kwa mujibu wa Harmonize, albamu hii ya sita ameiandaa kwa utulivu mkubwa kiasi kwamba anaamini ina hadhi ya kushinda tuzo kubwa za muziki duniani za Grammy ambazo zimekuwa zikitolewa Marekani tangu mwaka 1959.

Utakumbuka mwaka uliopita, baadhi ya wanamuziki wa Bongofleva waliotoa albamu ni Darassa (Take Away The Pain), Jay Melody (Addiction), Lady Jaydee (Silver) ambayo ilikuwa albamu yake ya 10.

Upande wa EP kuna Jux (A Day To Remember), Mbosso (Room Number 3), Nedy Music (The Voice of The Island), Lava Lava (Time), Yammi (After All), Phina (Melanin Therapy) ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2018.