Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne za Harmonize zapenya Grammy

HERMONIZE Pict

Muktasari:

  • Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo ameonesha furaha yake kuingiza nyimbo nne katika hatua hiyo.

Nyimbo nne alizoshiriki mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize, zimeingia na kutambuliwa na Grammy Academy kwa ajili ya hatua ya kwanza ya mchujo 'Consideration' katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Februari 1, 2026.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo ameonesha furaha yake kuingiza nyimbo nne katika hatua hiyo.

Nyimbo hizo ni Me Too ft Abigail Chams, Simuoni aliyoshirikishwa na AY, Furaha, na Finally aliyomshirikisha Miri Ben-Ari. Nyimbo zote nne zimewasilishwa kwenye Kipengele cha Best African Music Perfomance.

HERMO 01

Utakumbuka kwenye hatua hiyo Harmonize ameingia na msanii wa Hip hop, Fid Q ambaye ameandika historia hiyo mpya baada ya wimbo wake unaopatikana kwenye albamu yake ya Kitaa Rejex iliyotoka 2025, Glory 2 aliomshirikisha Damian Soul na Jose Chameleone kuingizwa katika mchujo wa Tuzo za Grammy.

Pia, nyimbo mbili za mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, AY zimeidhinishwa na kupitishwa rasmi na Grammy Academy kwa ajili ya mchakato unaofuata wa kuteuliwa kwenye vipengele vya tuzo hizo. Nyimbo za AY zilizofanikiwa kupenya kwenye hatua hiyo ni Simuoni aliyomshirikisha Harmonize, na Wanganeka ft Kanjiba.

HERMO 02

Baada ya hatua hiyo, nyimbo zilizofanikiwa kupenya kwenye Consideration ya Grammy zinapigiwa kura na kamati ya Grammy Academy kwaajili ya kuingia kwenye vipengele 'Nomination' za tuzo hizo.

Upigaji wa kura ulianza Oktoba 3, 2025 na utamalizika Oktoba 15, 2025, nyimbo na wasanii watakaowania vipengele vya tuzo hizo watatangazwa Novemba 7, 2025, wakati tuzo za 68 za Grammy zinatafanyika Februari 1, 2026.