Chriss amtunuku Kurrueche
Muktasari:
Pete hiyo iliyonakishiwa kwa madini ya almasi imeonekana kutulia vyema kwenye kidole cha Kurrueche aliponaswa na mwandishi wa Mtandao wa TMZ.
MUDA mfupi baada ya kuzagaa uvumi wa kuachana na kurudiana, mwanamuziki Chris Brown amempatia zawadi ya pete ya thamani mpenzi wake Kurrueche.
Pete hiyo iliyonakishiwa kwa madini ya almasi imeonekana kutulia vyema kwenye kidole cha Kurrueche aliponaswa na mwandishi wa Mtandao wa TMZ.
Hata hivyo, Kurrueche hakutaka kufafanua juu ya pete hiyo zaidi ya kueleza kuwa amepewa na Chris Brown.
Hivi karibuni wawili hao walionekana wakila bata pamoja kwenye klabu moja ya usiku huko Hollywood.