Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cardi kutoka kimapenzi na kipa

CARDI Pict

Muktasari:

  • Rapa huyo ambaye amekuwa akihusishwa kutoka na mastaa tofauti, amesema maisha yake yamekuwa chini ya uangalizi mkubwa kiasi kwamba kila anachofanya hugeuka kuwa habari.

RAPA maarufu wa Marekani, Cardi B amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikimuhusisha kutoka kimapenzi na kipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Maduka Okoye.

Rapa huyo ambaye amekuwa akihusishwa kutoka na mastaa tofauti, amesema maisha yake yamekuwa chini ya uangalizi mkubwa kiasi kwamba kila anachofanya hugeuka kuwa habari.

Akizungumza kuhusu uvumi huo, Cardi B amesema anashangazwa na namna maisha yake binafsi yanavyofuatiliwa zaidi tofauti na mastaa wengine duniani.

“Najua mastaa wengi wanakuwa kwenye mahusiano lakini hakuna anayeyaandika. Lakini ikija kwangu, siwezi hata kukojoa kwenye kikombe lazima itakuwa habari,” amesema Cardi B akimaanisha kila anachofanya lazima kisambae mitandaoni.

CARD 01

Kauli hiyo imekuja baada ya yeye na Okoye kuonekana pamoja mara kadhaa katika miji ya Ufaransa na Italia, jambo lililoibua maswali kutoka kwa mashabiki kuhusu aina ya uhusiano uliopo kati yao.

Kuhusishwa kwa wawili hao kulianza miezi miwili iliyopita baada ya kuonekana wakiondoka pamoja katika hafla ya mitindo jijini Paris na baadae mwenyewe Cardi B kumsifia kipa huyo kuwa ana muonekano mzuri.

Siku chache baadaye walionekana tena wakitumia muda pamoja wakati wa mapumziko nchini Italia, huku picha na video zao zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.