Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BET AWARDS 2026: Teyana Taylor, Clipse watawala, lamar kama kawa, waafrika hoi

Muktasari:

  • Teyana na Clipse kila mmoja waliondoka na tuzo tatu wakiweka histori nyingine ya kuchukua tuzo nyingi zaidi usiku huo uliohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki, filamu, michezo na burudani kutoka sehemu mbalimbali duniani.

LOS ANGELES, MAREKANI: TOLEO la 26 la Tuzo za BET Awards limeacha historia duniani baada ya kushuhudia ushindani mkali kutoka kwa mbalimbali wakiwemo wa muziki huku Teyana Taylor na kundi la Clipse wakitwaa tuzo nyingi zaidi usiku huo katika hafla iliyofanyika Peacock Theater, Los Angeles, Marekani.

Teyana na Clipse kila mmoja waliondoka na tuzo tatu wakiweka histori nyingine ya kuchukua tuzo nyingi zaidi usiku huo uliohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki, filamu, michezo na burudani kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Katika tuzo hizo, nyota kutoka Afrika, Wizkid, Burna Boy, Tems na Asake wakiondoka patupu licha ya kuingia katika vinyang’anyiro tofauti.

Mbali na tuzo hizo tatu, Teyana pia alipewa tuzo maalumu ya Icon of the Year, ikiwa ni heshima ya kutambua mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki na filamu.

Tuzo hizo ziliongozwa na mchekeshaji maarufu, Druski, huku zikishuhudia ushindani mkubwa katika vipengele mbalimbali kutokana na wasanii wengi wakubwa kuwania tuzo hizo.

Kundi la Clipse lilionyesha ubora wake baada ya kushinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kupitia albamu yao ‘Let God Sort Em Out’. Mbali na hilo, kundi hilo lilitwaa pia tuzo ya Kundi Bora pamoja na tuzo ya Ushirikiano Bora kupitia wimbo ‘Chains & Whips’ waliomshirikisha rapa Kendrick Lamar.

Kwa upande wa Kendrick Lamar, licha ya kushinda tuzo ya Ushirikiano Bora akiwa na Clipse, pia aliandika historia mpya baada ya kutwaa tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Hip Hop kwa mara ya tisa katika maisha yake, jambo linalomfanya kuwa msanii aliyeshinda tuzo hiyo mara nyingi zaidi.

Teyana ambaye ni raia wa Marekani alishinda tuzo ya muigizaji bora wa kike, mwongozaji bora wa video na tuzo mpya ya Fashion Vanguard Award.

Ni mwaka wa mafanikio kwa Teyana ambaye mwaka huu pia alishinda tuzo ya Golden Globe, kuteuliwa kwenye tuzo za Oscar na kuwania tuzo ya Grammy kupitia albamu yake ya Escape Room ingawa hakufanikiwa kuchukua tuzo.

Mwanadada huyo aliyeanza karia yake ya burudani mwaka 2006 akiwa na miaka 15 kama dansa na baadae kugeukia kwenye muziki, filamu na tasnia nyingine.

Kazi yake ya kwanza kuonekana kideoni ilikuwa mwaka 2006  ambapo alifanikiwa kushiriki kwenye ngoma ya mwanamuziki, Beyonce ‘Ring the Alarm’ kama dansa na kumfungulia milango mingine kwenye kazi yake.

Mwimbaji Kehlani aliibuka na tuzo mbili za msanii bora wa kike wa R&B/Pop na video bora ya mwaka kupitia video ya wimbo wake Folded.

Katika kipengele cha msanii bora wa kike mwanadada huyo alikuwa anawania tuzo hiyo na Mnigeria, Tems, Olivia Dean, Camila Cabello, Coco Jones, Ari Lennox, Ella Mai Mariah the Scientist, Jill Scott na SZA.

Video bora ya mwaka ilizishinda ngoma za wasanii mbalimbali ikiwemo Kendrick Lamar akimshirikisha SZA ‘Luther’, Tyla ‘Channel’, Ella Mai ‘100’ ‘Anxiety’ ya Doechii, Escape Room (Short Film) ya Teyana na nyinginezo.

Msanii Cardi B alishinda tuzo ya msanii bora wa kike wa Hip Hop, ikiwa ni mara yake ya tatu kushinda tuzo hiyo tangu aanze kubeba mwaka 2018.

Kipengele hicho alikuwa anachuana na marapa wengine,Coi Leray, Doechii, Doja Cat, GloRilla, Latto, Megan Thee Stallion, Monaleo na YK Niece.

Mambo yalikuwa tofauti baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya manii bora wa kiume wa R&B/Pop ambapo tuzo hiyo ilikwenda kwa Leon Thomas aliyeandika historia ya kushinda kwa mara ya kwanza.

Wengi waliamini pengine tuzo hiyo ingeenda kwa Chris Brown, Bruno Mars au Usher ambao walipewa nafasi kubwa ya kushinda.

Olivia Dean naye alishinda tuzo ya msanii bora chipukizi ikiwa siku chache nyuma nyota huyo kushinda kipengele hicho kwenye tuzo za Grammy.

Kwa upande wa filamu, kazi ya Sinners ilinyakua tuzo ya Filamu Bora, huku nyota wake Michael B. Jordan akiondoka na tuzo ya muigizaji bora wa kiume.

Tuzo hizo pia zilitambua mchango wa watu mbalimbali katika burudani, ambapo gwiji wa muziki Lauryn Hill alitunukiwa tuzo maalumu ya Living Legend Icon Award, huku mtendaji mkongwe wa muziki Sylvia Rhone akipewa tuzo ya Ultimate Icon Award.