Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ariana Grande atangaza kujiondoa mitandaoni

Muktasari:

  • Grande ametangaza hayo kupitia mwakilishi wake baada ya kumaliza ziara yake ya Eternal Sunshine Tour ambayo amesema atajiondoa mitandaoni kwa muda.

MWANAMUZIKI na muigizaji wa Marekani, Ariana Grande, amesema kuanzia sasa atajiweka mbali na mitandao ya kijamii na maisha ya umaarufu akishindwa kufafanua ni sababu ipi hasa imemfanya kufikia uamuzi huo.

Grande ametangaza hayo kupitia mwakilishi wake baada ya kumaliza ziara yake ya Eternal Sunshine Tour ambayo amesema atajiondoa mitandaoni kwa muda.

Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya kuachiwa kwa video ya wimbo wake mpya wa 'Petal' ambayo imezua mjadala mkubwa mitandaoni kuhusu muonekano wake wa mwili ambapo sasa amepungua zaidi tofauti na awali.

Licha ya kutotaja sababu ya kwanini anajiondoa kwenye mitandao ya kijamii, lakini baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihusisha hilo na muonekano wake wa sasa. Hata hivyo, Grande amesema uamuzi huo hauhusiani na video ya wimbo wake iliyotoka.

“Uamuzi wa kuchukua hatua nyuma kutoka kwenye maisha ya hadharani ulikuwa umepangwa kwa muda mrefu,” amesema, akisisitiza kuwa si jambo alilolifanya kwa hasira au kutokana na presha ya siku chache.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kuzungumziwa kuhusu muonekano wake kwani mwaka 2013 akiwa na miaka 20, aliwahi kujibu kuhusu uvumi wa mabadiliko ya mwili wake.

Hata mwaka 2025 wakati wanazindua filamu mpya ya 'Wicked For Good' na mwigizaji mwenzake Cynthia Erivo, mjadala kuhusu mwili wake ulizuka tena huku mashabiki wakiuliza nyota huyo amepatwa na shida gani ni tatizo la kiafya au kuna nini kinaendelea.

Mwanadada huyo aliyezaliwa mwaka 1993, Florida nchini Marekani alianza kuimba akiwa na miaka 14 na albamu yake ya kwanza aliitoa mwaka 2008 ikiitwa 'I was Like'.

Tangu hapo, amekuwa miongoni mwa nyota wanaofuatiliwa zaidi nchini Marekani kuanzia kazi zake na hata maisha nje ya muziki.

Moja ya ngoma maarufu ya Grande ni 'One Last Time' iliyoachiwa miaka 11 iliyopita ambayo hadi sasa inafanya vizuri ikiwa na watazamaji zaidi ya milioni 600 kwenye mtandao wa Youtube.

Ukiachana na filamu ya 'Wicked for Good', alionekana kwenye filamu ya katuni ya 'Sam and Cat' iliyotoka mwaka 2013.

Hapo ndipo mjadala kuhusu muonekano wake ulivuma kwa kasi ndipo kipindi hicho mwaka 2013 akaamua kujibu akisema kuna njia nyingi za kuonekana mwenye afya na mrembo.