Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawavuruga wapinzani kwa pasi matata uwanjani

Muktasari:

  • Tangu Pep Guardiola alipoibuka na ile staili yake ya kupiga pasi nyingi uwanjani, tiki-taka mwaka 2008, jambo hilo limeifanya karibu kila timu ya soka katika dunia ya sasa kujaribu kutaka kucheza kama staili hiyo iliyokuwa ikichezwa na Barcelona enzi ya zama za kocha huyo.

LONDON, ENGLAND

MPIRA pasi unaambiwa.

Huo ndio mpango wa soka la kisasa. Unamiliki mpira na kumkaba mpira kwa staili ya kupiga pasi. Hilo ndilo soka la dunia ya leo.

Tangu Pep Guardiola alipoibuka na ile staili yake ya kupiga pasi nyingi uwanjani, tiki-taka mwaka 2008, jambo hilo limeifanya karibu kila timu ya soka katika dunia ya sasa kujaribu kutaka kucheza kama staili hiyo iliyokuwa ikichezwa na Barcelona enzi ya zama za kocha huyo.

Bahati mbaya ni kwamba timu nyingi zilizojaribu kuiga mfumo huo, zinashindwa kuufanya kwa ubora kama inavyofanya Barcelona. Mhusika wa mtindo huo ni Guardiola, ambao aliupeleka pia Bayern Munich huko Ujerumani alipokwenda kuwanoa kabla ya sasa kutesa nao kwenye Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Manchester City. Soka la kupiga pasi nyingi hadi mpinzani anachanganyikiwa.

Tofauti ya Guardiola na makocha wengine ni kwamba pasi zake anazotaka zipigwe na wachezaji wake, anataka wafanya hivyo kwenye nusu ya timu pinzani, yaani kwenye eneo la kushambulia na si kupiga pasi kwenye eneo lao. Ligi Kuu England msimu huu imeshuhudia mastaa kibao hatari kwa kupiga pasi na hawa ndiyo waliopiga pasi nyingi zaidi katika eneo la wapinzani katika ligi hiyo.

Mesut Ozil - Arsenal, pasi 1181

Huduma bora ya kiungo huyo Mjerumani ndiyo iliyomfanya Arsene Wenger kukubali kumpa mkataba mpya na mshahara wa kibosi. Mesut Ozil kwa sasa analipwa mshahara usiopungua Pauni 300,000 kwa wiki kutokana na huduma yake anayotoa huko Emirates. Ozil ni fundi wa kupiga pasi na kwenye Ligi Kuu England msimu huu amepiga pasi 1181 katika nusu ya timu ya wapinzani. Ozil aliripotiwa kupata majeraha siku za karibuni akiwa kwenye kikosi chake cha Timu ya Taifa ya Ujerumani na hivyo kushindwa kuitumikia timu hiyo katika mechi za kimataifa.

Fernandinho - Man City, pasi 1212

Kimfumo Fernandinho anasimama mbele ya mabeki wa kati kwenye kikosi cha Manchester City kuhakikisha hakuna madhara yanayoelekezwa kwenye goli lao. Lakini, kutokana na mtindo wa kiuchezaji wa Kocha Guardiola, Fernandinho anatimiza majukumu yake ya kukaba kwa kupiga pasi, huku akiihamisha timu pinzani katika nusu yao. Kutokana na hilo, ndio maana Mbrazili huyo ni miongoni mwa wakali waliopiga pasi nyingi wakiwa kwenye nusu ya timu ya wapinzani kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Pasi 1212.

David Silva - Man City, pasi 1272

Fundi wa mpira kutoka Hispania. David Silva ni mmoja kati ya wachezaji wanaovutia kuwatazama ndani ya uwanja wakati mipira inapokuwa kwenye miguu yao. Kwa mtindo wa Guardiola ni jambo analofurahia kweli kweli kwenda kukutana na huduma ya Silva huko kwenye kikosi cha Man City. Mara kadhaa Guardiola amekuwa akimtumia Silva kwenye nafasi ya kiungo mkabaji, lakini amekuwa akiwateketeza wapinzani kutokana na pasi zake matata na ndio maana Mhispaniola huyo amepiga pasi 1272 kwenye nusu ya wapinzani katika mechi za Ligi Kuu England alizocheza msimu huu.

Kevin De Bruyne - Man City, pasi 1337

Anapigiwa upatu kuwa ndiye mchezaji anayestahili kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Ligi Kuu England msimu huu. Hilo linatokana na namna anavyowavuruga wapinzani na kupiga pasi za mwisho ambazo zinawafanya kupata mabao na hivyo Manchester City kuwa tishio kwe nye ligi wak iongoza kwa gepu kubwa la pointi baina yake na Manchester United wanaoshika nafasi ya pili. De Bruyne ukiacha zile pasi zake za mwisho zinazoleta mabao, ametawala zaidi kwenye eneo la wapinzani baada ya kupiga pasi 1337 katika nusu ya timu ya wapinzani katika mechi alizocheza katika Ligi Kuu England msimu huu.

Granit Xhaka - Arsenal, pasi 1351

Wanasema nabii hakubaliki kwao. Kama kuna mchezaji ambaye ukiwauliza mashabiki wa Arsenal wanamchukuliaje kama watatakiwa waamue kumuuza au kumbakiza, wengi watakwambia auzwe tu.

Huyu ni Granit Xhaka, lakini kitu anachokimiliki na namna anavyoifanya timu hiyo ya Arsenal kuondoka kwenye eneo lake na kwenda kutawala nusu ya timu pinzani kinamfanya abaki kuwa bora jambo mchango wake umekuwa hauonekani sana. Xhaka ni kiungo ambaye ameifanya Arsenal kuwa hai kwenye nusu ya wapinzani wao kutokana na kuwa mchezaji aliyepiga pasi nyingi zaidi kwenye eneo hilo kuliko mchezaji yeyote kwenye Ligi Kuu England. Xhaka amepiga pasi 1351 na kuifanya Arsenal kutamba kwenye eneo la timu pinzani ndani ya uwanja.