Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaiwahi Singida United

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza safari yake kwenda Singida kesho Ijumaa kwa ajili ya mechi yao ya robo fainali Kombe la Shirikisho dhidi Singida United itakayopigwa Jumapili ambayo ni Sikukuu ya Pasaka.

Wachezaji wa Yanga waliokuwa kambini na timu ya Taifa, Taifa Stars, jana walitarajiwa kusafiri kuelekea mkoani Morogoro kujiunga na wenzao.

Nyota hao waliokuwa wanatarajiwa kujiunga kambini na wenzao hiyo jana ni pamoja na Ibrahim Ajib, Hassan Kessy, Kelvin Yondan na Gadiel Michael ambao awali walikuwa kwenye timu ya Taifa.

Yanga imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo watakuwa wageni wa Singida United kwenye Uwanja wa Nafua.

Hata hivyo mlinda mlango Ramadhan Kabwili, ameshindwa kujiunga na timu yake ya Yanga kutokana na kuitumikia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inayojiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea Afcon U20.