Timbe apata ulaji China

Muktasari:

Heilongjiang walipandishwa msimu huu kutoka daraja la pili. Wanaandaa mechi zao za nyumbani katika uga wa Harbin ICE Centre unaomiliki idadi ya mashabiki 50 000.

 

Nairobi. Winga wa Harambee Stars, Ayub Timbe amejiunga na klabu ya daraja la kwanza Uchina Heilongjiang Lava Spring FC japo kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Beijing Renhe.

Timbe (25) alijiunga na Renhe mapema msimu jana wakiwa daraja la kwanza na kuwasaidia kupanda ligi kuu ya msimu huu. Hata hivyo, baada ya kufunga magoli manane na kuchangia matatu kwenye mechi 23 msimu jana, alikumbwa na jeraha la kisigino Oktoba.

Ni hilo jeraha linamsumbua hadi sasa hivi jambo lililowafanya Renhe kumpa kwa mkopo ili kujaza nafasi yake na nyota mwingine atakayewasaidia pindi tu msimu utaanza mwezi Aprili.

Timbe anatarajiwa kurejea fiti mwezi Juni.

“Tulionelea akahamie klabu nyingine sababu Renhe walikuwa wanamshinikiza kuanza matayarisho ya kabla ya msimu wakati anaumwa,

“Ni uhamisho utakaompa muda wa kupona sababu klabu hii ilielewa hali yake na akipona tu atawasaidia,” alisema nduguye Shaban Masika.

Heilongjiang walipandishwa msimu huu kutoka daraja la pili. Wanaandaa mechi zao za nyumbani katika uga wa Harbin ICE Centre unaomiliki idadi ya mashabiki 50 000.