Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars yawachezesha ndombolo Wacongo

Muktasari:

Taifa Stars ikicheza mchezo wa pili uliomo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ilitoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

Dar es Salaam. Mbinu ya kujaza idadi kubwa ya wachezaji wa kiungo, kushambulia kupitia pembeni kumeipa manufaa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kimataifa dhidi ya DR Congo.

Taifa Stars ikicheza mchezo wa pili uliomo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ilitoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

Mchezo huo ni maalumu ukiwa ni wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Tofauti na mchezo wa awali walionyukwa mabao 4-1 na Algeria mjini Algiers, Stars ilicheza soka ya uhakika na kuwapa raha Watanzania.

Mabao mawili ya nahodha Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na Shiza Kichuya yalizima ‘ndombolo’ la Wacongo hao. Samatta amefikisha mabao 15 katika mechi 40 alizocheza tangu mwaka 2011 na Taifa Stars.

Kocha Salum Mayanga, alianza kwa kuwatumia viungo watatu Erasto Nyoni, Himid Mao na Mohammed Issa ambao walisimama imara katika dimba la kati.

Kipa Aishi Manula aliyekuwa langoni katika mchezo wa jana, Nyoni na Issa hawakuanza mchezo uliopita dhidi ya Algeria.

Nyoni na Himid walifanya kazi nzuri ya kuchezesha timu kusaidia safu ya ulinzi iliyoundwa na mabeki wa pembeni Shomari Kapombe, Gadiel Michael huku Abdi Banda na Kelvin Yondani wakicheza katikati.

Mchezo ulivyokuwa

Dakika 10 za kipindi cha kwanza Taifa Stars ilianza kutafuta mabao ya kushitukiza, Samatta na Saimon Msuva wakiisumbua ngome ya DR Congo iliyokuwa chini ya mabeki Glody Ngoda na Yannick Bangala.

Muda ulivyokuwa ukisogea Taifa Stars ilibadilika kwa kushambulia lango la DR Congo kupitia upande wa kulia aliokuwa akicheza Kichuya.

Kiungo huyo wa pembeni alikuwa msumbufu kwa mabeki wa DR Congo na mara kadhaa aliwatoka kabla ya kumimina krosi kwa Samatta au Msuva.

Ibrahim Ajibu aliyeingia kuchukua nafasi ya Issa, aliongeza kasi ya mashambulizi yaliyowapa kazi ya ziada mabeki wa DR Congo.

Kichuya alifanya kazi nzuri kwa kutengeneza bao dakika ya 74 kwa kuchonga mpira wa krosi iliyomkuta Samatta aliyefunga kwa kichwa.

Kabla ya kufunga, mshambuliaji huyo alisogea haraka langoni kwa DR Congo na kuwazidi ujanja mabeki kabla ya kupiga mpira kichwa.

Mayanga alimtoa Himid na kuingia, Mudathir Yahya ambaye aliongeza nguvu kwa kulisakama lango la DR Congo na dakika ya 85 Taifa Stars ilipata bao la pili lililofungwa kwa shuti kali la mguu wa kushoto na Kichuya.