Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nchi 11 kushiriki mashindano ya kanda

Arusha: Tanzania imepewa jukumu la kuandaa na kuwa wenyeji wa mashindano ya riadha ya vijana ya ukanda wa tano yatakayofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 3 hadi 4.

Mjumbe wa Kamati ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo alisema kuwa kamati ya ufundi iliyokaa juzi jumatano ilimteua Robert Kalyahe na Mwinga Mwanjala kuwa makocha wa timu hiyo itakayoingia kambini wiki mbili kabla ya mashindano.

“Mwishoni mwa wiki kutakuwa na mashindano ya wazi hapa Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa na kazi ya kwanza wataanzia hapo kusaka wachezaji wa timu hiyo,” alisema Chambo.

Aliongeza kuwa imekuwa fahali kwa Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano hayo makubwa mfululizo kwa kuwa mwaka jana pia Tanzania ilikuwa wenyeji na kufanikisha kwa ustadi mkubwa.

Timu hiyo inatarajia kuwa na wanariadha wasiozidi 20 na wasiopungua 15 ambao na watakuwa katika makundi tofauti kwa wanariadha wanaokimbia kuanzia 100 mita hadi 10,000 mita.

Nchi zinazounda ukanda wa tano ni pamoja na Tanzania, Zanzibar, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan, Sudan Kusin, Eritrea, Djibouti, Burundi na Somalia.