Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchezaji feki awapoza Bunda Town Star

Mwanza. Kamati ya Mashindano ya Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) kimeipokonya ushindi timu ya Bunda Town Stars baada ya kubainika kumchezesha mchezaji aliyeghushi leseni wakati wa mchezo wao dhidi ya Nyamongo FC.

Katika mchezo uliopigwa Jumanne ya wiki iliyopita, Bunda ilishinda kwa changamoto ya penalti mabao 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kutinga fainali.

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoani humo, Samwel Silas alisema kuwa Bunda Town walimchezesha mchezaji Patrick Petro aliyetumia leseni ya Ramadhan Kitundu, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za mashindano.

Alisema kuwa katika kikao walichoketi jana Jumanne kupitia rufaa ya timu ya Nyamongo walibaini Bunda Town kumchezesha kimakosa mchezaji huyo ambaye alikuwa hana usajili.

 

“Kamati ya Mashindano ilikaa Jumanne (juzi) kupitia rufaa ya Nyamongo waliopinga dhidi ya Bunda Town kumchezesha mchezaji ambaye hakuwa na usajili, tulipofuatilia tumebaini ni kweli, hivyo tumeipokonya ushindi,” alisema Silas.

Katibu huyo alisema kuwa kutokana na maamuzi hayo, Nyamongo ndio wanatinga fainali na watakutana dhidi ya Mara United, mchezo utakaopigwa leo Alhamisi.