Liverpool yatua na kikosi kamili Ukraine

Kiev. Kikosi cha Liverpool tayari kimetua Kiev, Ukrain ambako kitacheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kesho Jumamosi.

Mamia ya mashabiki walifurika nje ya hoteli ambayo wamefikia wachezaji hao ili kuwakaribisha.

Kikosi cha mashabiki hao kilipokewa kwa shangwe na mashabiki ambao walikuwa wameshika mabango kuipa hamasa kuweka hiostoria yake ya soka kwenye makao hayo makuu ya Ukraine.

Kocha wa timu hiyo alizawadiwa zawadi ya kiutamaduni ya nchi hiyo wakati akiwasili pamoja na wachezaji wake jana Alhamisi jioni.

Awali, mashabiki wengine walijitokeza kwenye Uwanja wa Ndege na kusalimiana na mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah pamoja na kumkabidhi zawadi ya maua.