Ishu ya Man United, Griezmann imefika hapa

Muktasari:

Wakati hali ikiwa hivyo, taarifa mpya ni kuwa wababe hao wa Old Trafford wamefuta mpango wa kumsajili straika wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann na badala yake wametua kwa winga wa Real Madrid, Gareth Bale.

MAMBO ni magumu na hali ya sintofahamu kuhusiana na mustakabali wa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, imeendelea kushika kasi pale Old Trafford.

Wakati hali ikiwa hivyo, taarifa mpya ni kuwa wababe hao wa Old Trafford wamefuta mpango wa kumsajili straika wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann na badala yake wametua kwa winga wa Real Madrid, Gareth Bale.

Kwa muda mrefu sasa, Man United imekuwa ikimuwinda Griezmann, ambaye kuna wakati ilitangazwa wamefikia makubaliano binafsi, lakini kwa sasa mambo yamebadilika na staa huyo wa Kifaransa anatajwa anaweza kutua Barcelona mwishoni mwa msimu huu.