Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga mikononi mwa CAF

Muktasari:

Yanga ambao ni mabingwa watetezi, watacheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba Kombe la Shirikisho mwaka huu.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), linatarajiwa kutuma maofisa kuja nchini kukagua miundombinu ya uwanja wa mazoezi utakaotumiwa na timu za Simba na Yanga.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi, watacheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba Kombe la Shirikisho mwaka huu.

Ofisa Habari wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema maofisa hao watakagua maeneo mbalimbali ya uwanja.

“CAF wanataka kuhakikisha viwanja vyote vinakuwa kwenye viwango vya juu, namaanisha vitakavyotumiwa na timu zetu za nyumbani ambazo ni Simba na Yanga.

“Siku yoyote watatupa taarifa lini watawasili kwa ukaguzi huo na jambo la muhimu Simba na Yanga ni kujiandaa kwa ukaguzi huo,” alisema Ndimbo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema wanasubiri ujio wa CAF kwasababu hawana shaka kuhusu ubora wa uwanja watakaotumia.

“Tulipata taarifa ipo siku maofisa wa CAF watafika haya ni mashindano makubwa Afrika lazima ufanyike ukaguzi wa uwanja kabla ya kutumika.

“Uwanja wetu ambao tutatumia kama wa nyumbani ni Taifa, mazoezi tutatumia Uwanja wa Uhuru,” alisema katibu huyo ambaye pia kitaaluma ni kocha.

Yanga itavaana na mabingwa wa Shelisheli, Port Louis na ikisonga mbele itapepetana na mshindi baina ya El Merreikh au Township Rollers.

Simba imepangwa kuanza na timu ya Gendarmerie Nationale ya Djibout na ikifanikiwa kufuzu hatua hiyo itaumana na mshindi baina ya Al-Masry na Green Buffaloes.