Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Simba awapa Yanga kiungo

Muktasari:

Kikosi cha Yanga kinaendelea kusaka wachezaji kutoka katika maeneo mbalimbali Afrika na kiungo wa Rayorn Sport ya Rwanda Ally Niyonzima ni miongoni mwao.

KOCHA wa zamani wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Mnyarwanda Masoud Djuma amesama kama kweli Yanga wanataka kumsajili kiungo wa Rayon Sports FC, Ally Niyonzima ni mchezaji mzuri.
Djuma amesema amekuwa akisikia taarifa hizo kupitia mitandao mbalimbali kuhusu Niyonzima kujiunga na Yanga.
Anasema mchezaji huyu aliwahi  kumfundisha klabu ya AS Kigali 2017/18, na alikuwa akimtumia kikosi chake cha kwanza.
"Niyonzima nilikuwa nikimtumia katika nafasi tatu tofauti uwanjani kutokana na umahiri wake ambao alikuwa akionesha kwenye timu,".
"Kama kweli Yanga wanataka kumsajili mchezaji huyu ni mzuri ambaye ataimarisha timu yao eneo la kiungo na kuwa bora zaidi.
"Niyonzima anaweza kucheza nafasi nyingine kama mlinzi wa kati au mshambuliaji (namba 10), kwa maana hiyo kwangu Yanga kama watamsajili watakuwa wamepata mchezaji mzuri," amesema Djuma.