Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yoro Diaby atua Ufaransa, kunolewa na Gael Clichy

Muktasari:

  • Diaby, 25, amesaini kuichezea Caen inayoshiriki Championnat National, daraja la tatu nchini Ufaransa, baada ya kumaliza safari yake ya misimu miwili ndani ya kikosi cha Azam FC. Klabu ya Caen ilitangaza rasmi usajili wa beki huyo Septemba 11, 2026.

BEKI wa kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby, ameanza safari mpya ya maisha yake ya soka baada ya kutua Stade Malherbe Caen ya Ufaransa, ambako atakuwa chini ya mikono ya aliyekuwa beki wa Arsenal, Manchester City na timu ya taifa ya Ufaransa, Gaël Clichy.

Diaby, 25, amesaini kuichezea Caen inayoshiriki Championnat National, daraja la tatu nchini Ufaransa, baada ya kumaliza safari yake ya misimu miwili ndani ya kikosi cha Azam FC. Klabu ya Caen ilitangaza rasmi usajili wa beki huyo Septemba 11, 2026.

Clichy, beki aliyepata uzoefu mkubwa katika soka la kiwango cha juu akiwa Arsenal na Manchester City, pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa amegeukia kazi ya ukocha, ndiye anayesimamia benchi la Caen.

Diaby safari yake ya soka ilianzia Mali katika klabu ya Yeelen Olympique, kabla ya kuhamia Stade Malien.

Stade Malien ndiyo iliyokuwa daraja muhimu kwake kabla ya kuja Tanzania, huku uwezo aliouonyesha ukimfungulia mlango wa kujiunga na Azam mwaka 2024.

Akiwa Azam, Diaby alitumia misimu miwili, 2024-2025 na 2025-2026, akiwa sehemu ya kikosi cha matajiri hao wa Chamazi katika mashindano mbalimbali.

Mkataba wake ulipofikia ukomo 2025-2026, Azam ikatangaza kumuaga Diaby na kuanza kutafuta changamoto mpya, hatimaye amepata nafasi ya kutua Ulaya kupitia Caen.

Sasa beki huyo anaingia katika mazingira mapya akiwa na jukumu la kuisaidia Caen, ambayo inashiriki Championnat National, daraja la tatu nchini Ufaransa, katika harakati za kurejea Ligue 2.

Kwa upande wake, Diaby anataka kupata muda wa kutosha wa kucheza, kuonyesha uwezo wake mbele ya Clichy na kutumia fursa hiyo kujijenga zaidi katika soka la Ulaya.