Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xabi Alonso apigwa chini Real Madrid

ALONSO Pict

Muktasari:

  • Alonso alitumia miaka mitano na mabingwa hao wa Hispania kama mchezaji na kurejea klabuni hapo alipoteuliwa kuwa kocha mkuu majira ya joto mwaka huu.

MADRID, HISPANIA: XABI ALONSO ameachana na  Real Madrid siku moja baada ya kupoteza fainali ya Super Cup dhidi ya Barcelona. Taarifa ya klabu imesema uamuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 kuondoka ulifanywa kwa makubaliano ya pande mbili.

Alonso alitumia miaka mitano na mabingwa hao wa Hispania kama mchezaji na kurejea klabuni hapo alipoteuliwa kuwa kocha mkuu majira ya joto mwaka huu.

Hata hivyo, tayari ameshaachia madaraka baada ya kuongoza klabu hiyo kwa muda wa miezi sita tu.

Taarifa ya klabu hiyo imesema: “Real Madrid CF inatangaza kwamba, kwa makubaliano kati ya klabu na Xabi Alonso, imeamuliwa kumtangaza mwisho wa uhusiano wake kama kocha wa kikosi cha kwanza. 
“Xabi Alonso daima atakuwa na upendo na heshima ya mashabiki wa Madrid kwa sababu yeye ni mchezaji wa Real Madrid na daima amewakilisha maadili ya klabu yetu. 
“Real Madrid daima itakuwa nyumbani kwake. 
“Klabu yetu inamshukuru Xabi Alonso na timu yake yote ya ufundi kwa kazi na kujitolea kwao wakati huu, na inawatakia kila la heri katika hatua hii mpya ya maisha yao.”

Na Madrid hawakupoteza muda kutangaza nani atakuwa mrithi wake kwenye benchi la ufundi. Mchezaji wa zamani wa Real Madrid na mwenzake wa zamani wa Alonso, Alvaro Arbeloa, ametangazwa kuwa mrithi wake.

Arbeloa, ambaye alistaafu mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 34 baada ya msimu mmoja West Ham, alijiunga na benchi la  ufundi la Real Madrid mwaka 2020. Alitangazwa kuwa kocha wa Castilla Juni iliyopita na sasa ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya kwanza.

Hii inafanana na Zinedine Zidane mwaka 2016 alipotangazwa kuwa kocha wa timu ya kwanza baada ya kuinuliwa kutoka kuwa kocha wa Castilla.