Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenger ajitenga na Infantino

Muktasari:

  • Infantino mwenye umri wa miaka 56 alizua taharuki wiki iliyopita baada ya kuibuka kwa taarifa za mpango wa kuruhusu wawekezaji binafsi kununua hisa katika michuano ya Kombe la Dunia, hatua iliyokosolewa vikali na wadau wa soka duniani.

LONDON, ENGLAND: Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ameita kikao cha dharura nchini Morocco katika juhudi za kuokoa nafasi yake madarakani, huku shinikizo dhidi yake likizidi kuongezeka kufuatia mpango wake ulioshindikana wa kuuza hisa za Kombe la Dunia.

Infantino mwenye umri wa miaka 56 alizua taharuki wiki iliyopita baada ya kuibuka kwa taarifa za mpango wa kuruhusu wawekezaji binafsi kununua hisa katika michuano ya Kombe la Dunia, hatua iliyokosolewa vikali na wadau wa soka duniani.

Upinzani huo uliongozwa na UEFA pamoja na mashirikisho mengine ya mabara, ambayo yalitishia kususia Kombe la Dunia na hata kuanzisha mashindano mbadala yaliyolenga kuipokonya FIFA ushawishi wake.

Kutokana na presha hiyo, Infantino alilazimika kuufuta mpango huo, lakini sasa anakabiliwa na vita ya kubaki madarakani kabla ya uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika Machi mwakani.


WENGER AJITENGA NA INFANTINO

Pigo jingine kwa Infantino limekuja kutoka kwa mkuu wa maendeleo ya soka wa FIFA, Arsene Wenger, ambaye amesema hakuhusishwa kabisa na mpango huo na aliujua kupitia taarifa za vyombo vya habari.

Kocha huyo wa zamani wa Arsenal alisisitiza kuwa uamuzi wa kuufuta mpango huo ulikuwa sahihi.

"Uamuzi wa kuondoa mradi huo ulikuwa wa lazima kabisa. Ninaamini FIFA inapaswa kubaki taasisi huru inayohudumia mchezo kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji," alisema Wenger.


KIKAO CHA DHARURA MOROCCO

Kwa mujibu wa taarifa, Infantino kwa sasa yupo Rabat, Morocco, ambako amewaita viongozi waandamizi wa FIFA kwenye kikao cha dharura kinacholenga kurejesha mshikamano ndani ya taasisi hiyo.

Inaelezwa pia kuwa viongozi waandamizi wa FIFA walifanya kikao kingine bila uwepo wa Infantino, ambapo karibu wote walipinga mpango huo wa kuuza hisa za Kombe la Dunia.


JORDAN YAMTUHUMU KWA 'BLACKMAIL'

Rais wa Shirikisho la Soka la Jordan, Prince Ali bin Al Hussein, amemshambulia vikali Infantino, akimtuhumu kutumia vitisho na ushawishi usiofaa ili kupata uungwaji mkono.

Kiongozi huyo alidai FIFA imechelewesha fedha zinazodaiwa kulipwa kwa Jordan baada ya kufika fainali ya Kombe la Waarabu nchini Qatar, huku akidai aliambiwa wazi kuwa kuunga mkono Infantino kungesaidia kutatua changamoto za shirikisho lao.

"Hii ni sawa na blackmail, na hatutakubali kushinikizwa kwa namna hiyo," alisema Prince Ali kupitia akaunti yake ya X.


KATIBU MKUU NAYE AVUNJA UKIMYA

Katibu Mkuu wa FIFA, Mattias Grafstrom, pia aliwatumia wafanyakazi wa shirikisho hilo barua pepe akieleza kusikitishwa na yaliyojitokeza, akisema matukio hayo hayapaswi kufifisha dhamira ya kuitumikia soka duniani.