Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiku wa vipingamizi, vigogo kuvurugana robo fainali UEFA CL

UEFA Pict

Muktasari:

  • Mechi mbili kati ya hizo zilikuwa ni zile za hatua ya mtoano ya 16 bora na PSG ilifanikiwa kupenya kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, mechi hii pia itaanza saa 4:00 usiku.

MADRID, HISPANIA: HATUA ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu rasmi itaanza leo na kuna jumla ya mechi za mkondo wa kwanza zitakazopigwa kule Hispania na Ureno.

Madrid itakuwa mwenyeji wa Bayern Munich katika mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kutokana na historia na ukubwa wa timu zote mbili.

Kwa jumla, timu hizi mbili zimekutana mara 26 katika michuano hii. Real Madrid imeshinda mechi 12, Bayern Munich imeshinda 11, na tatu zimemalizika kwa sare. Katika mabao, Real Madrid inaongoza kwa kufunga mabao 41 dhidi ya 39 ya Bayern Munich.

Katika hatua ya mtoano zimekutana mara 11 na kati ya hizo Madrid imefanikiwa kusonga mbele mara saba wakati Bayern ikisonga mara nne.

Katika robo fainali timu hizi zimekutana mara mbili na ni msimu wa  2003/04 na 2016/17 na mara zote Madrid ilisonga mbele.

Mbali ya mechi hii ambayo marudiano itakuwa ni April 15 katika viunga vya Allianz Arena kuanzia saa 4:00 usiku, mechi nyingine kwa leo itakuwa ni kati ya Sporting Lisbon dhidi ya Arsenal itakayopigwa huko Ureno.

Katika michuano ya Uefa, timu hizi zimekutana mara tano, mechi nne zikiwa ni za Europa League na kijumla na mbili ni zile za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal ndio ina takwimu nzuri zaidi kwani imeshinda mechi mbili, Leipzig imeshinda moja  kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Mechi hii inatarajiwa kuanza saa 4:00 usiku katika dimba la José Alvalade na mechi ya marudiano itapigwa katika viunga vya Fly Emirates muda kama huo, April 15.

Mbali ya mechi za leo, kesho pia michuano hii inatarajiwa kuendelea na kutakuwa na mechi mbili pia. Pale Nou Camp, Barcelona itakuwa inaikaribisha Atletico Madrid. Msimu huu timu hizi zimekutana mara nne katika michuano mbalimbali na Barca ameibuka na ushindi mara tatu, huku Atletico ikiwa ni mara moja.

Katika ligi ya mabingwa timu hizi zimekutana mara nne, zote zikiwa ni mechi za hatua kama hii ya robo fainali.

Kwanza kabisa ilikuwa msimu wa 2013/14 na Atletico ilifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1, pia zikakutana tena msimu wa 2015/16 na Atletico ikasonga mbele kwa tofauti ya mabao 3-2 baada ya mechi ya mkondo wapili kushinda mabao 2-0. Mechi hii itaanza saa 4:00 usiku.

Vilevile, kesho vijana wa Arne Slot, Liverpool ambao wanaonekana kupitia wakati mgumu, watashuka dimbani kuvaana na matajiri wa Jiji la Paris, PSG ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Tangu msimu wa 2018/19 timu hizi zimekutana mara nne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na hakuna mbabae kati yao kwani kila timu imeshinda mara mbili.

Mechi mbili kati ya hizo zilikuwa ni zile za hatua ya mtoano ya 16 bora na PSG ilifanikiwa kupenya kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, mechi hii pia itaanza saa 4:00 usiku.