Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England kupeleka timu saba UCL msimu ujao

Muktasari:

  • Mapema wiki iliyopita timu nne za Ligi Kuu England yaani Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur na Newcastle United zilitolewa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LONDON, ENGLAND: SHIRIKISHO la Soka Ulaya (Uefa) limethibitisha kuwa kuna uwezekano wa timu saba za Ligi Kuu England kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao lakini ikiwa mambo kadhaa yatatokea.

Mapema wiki iliyopita timu nne za Ligi Kuu England yaani Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur na Newcastle United zilitolewa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ni Arsenal na Liverpool pekee ndizo zilizofanikiwa kufuzu robo fainali ambapo Washika Mitutu wa London watakutana na Sporting CP wakati Majogoo wa Anfield wakivaana na Paris Saint-Germain katika hatua hiyo.

Licha ya matokeo mabaya ya timu zake ligi hiyo bado ina nafasi kubwa ya kupewa tiketi ya ziada ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao kupitia mfumo wa “European Performance Spot”.

Kawaida Uefa huzipa ligi mbili za juu zenye pointi nyingi katika michuano ya Uefa nafasi ya kuingiza timu moja ya ziada na hadi sasa England inaongoza kwa pointi 115.630 huku Italia ikiwa nafasi ya pili na pointi 99.660.

Hispania ipo nafasi ya tatu huku ushindi wa Aston Villa, Nottingham Forest na Crystal Palace katika Europa League na Conference League umeongeza nafasi ya England.

Ingawa bado haijathibitishwa kabisa kihesabu England kwa sasa ipo katika nafasi nzuri sana ya kupata faida ya kuingiza timu moja zaidi.

Msimu uliopita Newcastle walinufaika na nafasi hiyo ya ziada baada ya kumaliza watano katika msimamo.


SABA ZINAFUZU VIPI?

Ikiwa Aston Villa itashinda Europa League itapata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu wa 2026/27 kama ilivyokuwa kwa Tottenham msimu uliopita.

Liverpool au Arsenal zinaweza kufuzu moja kwa moja ikiwa moja kati yao itafanikiwa kushinda taji hilo.

Ikiwa hayo mambo mawili hapo juu yatatokea timu nyingine zitafaidika na kufanya idadi kufika saba kwani zitatakiwa klabu tano za kuungana na hizo mbili zilizofuzu moja kwa moja.

Kwa sasa Brentford ipo nafasi ya saba na inaweza ikawa moja kati ya timu zitakazofaidika na nyongeza ya idadi ya timu zitakazotakiwa kufuzu Uefa msimu ujao.

Kupitia taarifa yao Uefa ilithibitisha ikisema: “Iwapo Liverpool itashinda Ligi ya Mabingwa na kumaliza nafasi ya tano na Aston Villa ikashinda Europa League na kumaliza nafasi ya sita basi nafasi ya ziada (EPS) itatolewa kwa timu ya saba ya Ligi Kuu.”

Timu kama Brentford, Everton, Fulham, Brighton, Bournemouth, Sunderland na Newcastle zinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kufaidika.