Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usichokijua kuhusu kocha mpya Real Madrid

ARBELOA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi 262 walizocheza pamoja wakiwa Liverpool, Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, wawili hao walitumia zaidi ya dakika 20,000 uwanjani pamoja.

MADRID, HISPANIA: HAKUNA mtu aliyecheza mechi nyingi zaidi na kocha mpya wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa kuliko Xabi Alonso.

Katika mechi 262 walizocheza pamoja wakiwa Liverpool, Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, wawili hao walitumia zaidi ya dakika 20,000 uwanjani pamoja.

Hiyo ni sawa na kutumia karibu wiki mbili za maisha yao wakiwa kwenye uwanja wa mpira wakati wa mechi, bila hata kuhesabu muda waliotumia mazoezini au walipokuwa wakipumzika pamoja kama marafiki.

Hata hivyo, usitarajie Arbeloa kuwa aina ile ile ya kocha kama Alonso, ambaye alifukuzwa kazi Jumatatu baada ya kusimamia timu kwa mechi 34 tu.

Alonso, 44, alikuwa karibu kufukuzwa kabla ya Krismasi baada ya kutofautiana na baadhi ya wachezaji wake na kushindwa kabisa kujijenga upya kama kiongozi katika Uwanja wa Santiago Bernabéu.

Sasa, rafiki yake wa zamani, Arbeloa, 42, amechukuliwa kutoka kwenye akademi ya Madrid ili kuchukua mikoba yake ya kuinoa miamba hiyo inayofahamika kama Los Blancos.

Ikilinganishwa na Alonso, ambaye aliwahi kushinda Bundesliga akiwa na Bayer Leverkusen bila kupoteza mechi yoyote msimu mzima, akipoteza mechi moja tu kwenye fainali ya Europa League, Arbeloa bado anaonekana kama kocha mchanga.

ARBE 01

Amehusika na Real Madrid kwa zaidi ya miaka saba tangu alipostaafu soka akiwa West Ham mwaka 2017, lakini mchango wake mkubwa umekuwa katika ngazi za timu za vijana.

Beki wa kulia huyo wa zamani amepata mafanikio makubwa tangu aingie katika ukufunzi wa akademi ya Los Blancos, akishinda mataji matano katika miaka mitano katika vikosi vya umri mbalimbali, ikiwemo mataji matatu (treble) msimu wa 2022/23.

Hivi karibuni zaidi, Arbeloa alikuwa Kocha wa Real Madrid Castilla, timu ya akiba ya klabu, lakini bado hana uzoefu wa kuifundisha timu ya wakubwa.

Hiyo ni kama vile alivyokuwa Zinedine Zidane, ambaye aliibukia kutoka kwenye kikosi cha Real Madrid Castilla na kwenda kuiongoza Madrid ya wakubwa kutawala soka la Ulaya kwa njia ya kipekee mwishoni mwa miaka ya 2010.

Zidane alipandishwa kutoka Castilla hadi kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alonso alipitia timu ya akiba ya Real Sociedad kabla ya kupata kazi Leverkusen, na pia alikuwa na hadhi kubwa zaidi kama mchezaji, ingawa Arbeloa huenda hakuthaminiwa vya kutosha katika kikosi kilichojaa nyota. Kama ilivyokuwa kwa Alonso, Arbeloa pia alifanya kazi chini ya baadhi ya majina makubwa zaidi katika soka duniani.

Alitumia muda mwingi zaidi chini ya Jose Mourinho akiwa Madrid (mechi 122), huku Rafa Benitez akishika nafasi ya pili (mechi 102 katika vipindi vyake Liverpool na kwa muda mfupi Madrid).

Carlo Ancelotti yuko chini zaidi kwenye orodha hiyo, huku Manuel Pellegrini naye akihusika.

ARBE 02

Arbeloa hakuwa na muda mrefu sana wa kufanya kazi na Zidane, lakini bado alipata mazoezi na mechi chache chini ya gwiji huyo wa Ufaransa.

Je, hii inaashiria nini kuhusu namna Arbeloa atakavyoiongoza timu atakapoanza kazi rasmi na nyota kama Kylian Mbappé, Jude Bellingham, na Vinícius Jr?

Huenda jibu likapatikana kwenye mahojiano ya mwaka 2015 na gazeti la The Independent, badala ya kuchambua tu rekodi za timu za vijana za Madrid.

Katika mahojiano hayo, Arbeloa amesema kuhusu Mourinho, ambaye anamuenzi na kumheshimu sana: “Alikuwa kama kinga ya risasi kwa wachezaji. Kama mchezaji angekumbwa na lawama kutoka kwa wakosoaji, yeye alikuwa wa kwanza kumtetea. Alipambana na ratiba ya mechi; dhidi ya nyakati za kuanza mechi kama alihisi zinatuonea; au dhidi ya mwamuzi kama aliona ameitendea Real Madrid isivyo haki. Alipigania maslahi ya timu bila kujali kuwa mwisho wa siku taswira yake ingeathirika, ndipo akaitwa mlalamikaji.”

Ingawa Arbeloa ni shabiki mkubwa pia wa Benitez, alimpongeza Mourinho kwa kiwango cha juu sana, licha ya kuwa mpinzani wa zamani.

Aliongeza: “Kitu ambacho watu wengi hawazingatii wanapohukumu kipindi cha Mourinho nchini Hispania ni kwamba huenda kama asingekuja Madrid wakati ule, Guardiola angeendelea kushinda na Barcelona. Tulikuwa tunakabiliana na timu ambayo watu wengi huiita, kama si bora zaidi basi hakika moja ya bora zaidi katika historia. Na alikuwa akikabiliana na kocha kama Guardiola ambaye angeweza kubaki klabuni kwa miaka 25 kama Sir Alex Ferguson alivyokuwa Man United, ndivyo alivyokuwa akilingana kikamilifu na klabu hiyo, lakini Mourinho aliweza kuwashusha kutoka kileleni. Anastahili sifa za kutosha kwenye hilo.”