Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump, Infantino watangaza ahueni ya viza kwa mashabiki Kombe la Dunia

VISA Pict

Muktasari:

  • Mfumo huo utawezesha kupunguza muda wa kupata viza kwa mashabiki wanaopanga kuhudhuria fainali hizo zitakazounguruma nchini Mexico, Marekani na Canada kuanzia Juni 11, 2026.

Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, wametangaza mfumo mpya wa kurahisisha na kuharakisha mchakato wa kupata viza kwa mashabiki wanaopanga kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani.

Mfumo huo utawezesha kupunguza muda wa kupata viza kwa mashabiki wanaopanga kuhudhuria fainali hizo zitakazounguruma nchini Mexico, Marekani na Canada kuanzia Juni 11, 2026.

Mfumo huo utahakikisha mashabiki wanaopanga kwenda kuangalia mechi za Kombe la Dunia nchini Marekani watapewa kipaumbele katika kupata viza za utalii. Mchakato wa maombi na uhakiki bado ni uleule, lakini watafuta viza watapata miadi ya haraka zaidi.

VIS 01

Hata hivyo, shabiki atakayekuwa na tiketi ya mechi, hakutampa uhakika wa kuingia Marekani, bali kunasaidia kupata miadi ya haraka ya viza.

Trump na Infantino wanapendekeza kwamba kila mtu anayepanga kutembelea Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026 anapaswa kuanza mchakato huo mapema, badala ya kusubiri dakika za mwisho.

WC Pict

Gharama ya viza ya Marekani kwa raia wa Tanzania inatofautiana kulingana na aina ya viza wanayoiomba. Kwa mfano, viza ya wanafunzi (F-1) inagharimu takriban Dola za Marekani 265 (Sh649,250), wakati viza za mfanyakazi wa muda (H-1B) ni takriban Dola za Marekani 845 (Sh2 milioni).

Pia, baadhi ya viza zina malipo ya ziada yanayojulikana kama reciprocity fee, ambayo pia inategemea aina ya viza. Kwa Tanzania, malipo haya yameingizwa katika jumla ya gharama zinazotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani.