Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Soria: Ubelgiji inataka kuwa namba moja

SORIA Pict

Muktasari:

  • Soria aling’ara katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya New Zealand, Novemba 26, 2026, akifunga mabao mawili ndani ya dakika 20 za mwanzo za mechi hiyo na kuisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya vijana ya Ubelgiji chini ya miaka 17, Matteo Soria amesema ndoto yao ni kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA U-17, licha ya kukiri safari hiyo haitakuwa rahisi.

Soria aling’ara katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya New Zealand, Novemba 26, 2026, akifunga mabao mawili ndani ya dakika 20 za mwanzo za mechi hiyo na kuisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano.

Mshambuliaji huyo anayekipiga Club Brugge, amesema: “Tunataka kuwa namba moja. Itakuwa vigumu, lakini hilo ndilo tunalotaka kulifanya.”

SOR 01

Kocha wa Ubelgiji, Sven Vermant amesema alimpa Soria nafasi kwa sababu ana uwezo wa kufunga mabao na nguvu zinazohitajika kucheza nafasi ya ushambuliaji.

Amesema: “Yeye ni mshambuliaji na anajua kufunga mabao. Ana nguvu ya kucheza mbele. Ninaamini pia yuko tayari kucheza katika kiwango hiki pamoja na vijana waliozidi umri wake kwa mwaka mmoja.”

Safari ya Ubelgiji kufuzu hatua ya 32 bora ilianza kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Vietnam, kabla ya kupoteza 2-1 dhidi ya Mali, matokeo yaliyoiweka kwenye mazingira ya kutafuta ushindi katika mchezo wa mwisho ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Katika mchezo huo wa mwisho, Ubelgiji iliifumua New Zealand mabao 6-0. Ushindi huo uliifanya imalize Kundi G ikiwa nafasi ya pili kwa pointi sita, nyuma ya Mali iliyokusanya tisa na hivyo kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano.

SOR 02

Hata hivyo, safari ya Ubelgiji katika mashindano hayo ina historia ya muda mrefu, kwani ni mara yake ya nne kushiriki Kombe la Dunia U-17. Katika ushiriki wake wa mwaka 2007, ilitolewa hatua ya makundi, kabla ya kufanya vizuri zaidi mwaka 2015 nchini Chile ilipomaliza nafasi ya tatu na kutwaa medali ya shaba. Mwaka 2025 ilifika hatua ya 32 bora, hivyo safari ya mwaka huu inaipa nafasi nyingine ya kujaribu kuvuka rekodi hiyo.

Nahodha Preben Blondeel amesema kipigo cha fainali ya mashindano ya Ulaya U-17 mwaka huu dhidi ya Italia kwa mikwaju ya penalti, baada ya kuruhusu bao la kusawazishwa dakika za nyongeza, kimeongeza kiu ya kikosi hicho kufanya vizuri Qatar.