Senegal yafuzu AFCON 2027 kiulaini ikizichonganisha Msumbiji, Sudan
Muktasari:
- Kichapo cha bao 1-0 ambacho Ethiopia imekipata nyumbani kutoka kwa Msumbiji leo, Jumanne, Novemba 17, 2026 kimeifanya Senegal iwe na uhakika wa kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa kundi J na hivyo kujihakikishia tiketi ya kuwepo katika fainali hizo mwakani.
Senegal imekuwa timu ya kwanza ya Taifa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 zitakazofanyika Kenya, Uganda na Tanzania mwakani.
Kichapo cha bao 1-0 ambacho Ethiopia imekipata nyumbani kutoka kwa Msumbiji leo, Jumanne, Novemba 17, 2026 kimeifanya Senegal iwe na uhakika wa kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa kundi J na hivyo kujihakikishia tiketi ya kuwepo katika fainali hizo mwakani.
Senegal ambayo jana ilipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sudan, inaongoza msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi 10, ikifuatiwa na Msumbiji yenye pointi saba huku Ethiopia ikiwa nafasi ya tatu na pointi nne sawa na Sudan inayoshika mkia.
Bao pekee la Msumbiji ambalo limekuwa na faida kwa Senegal limefungwa na Stanley Ratifo katika dakika ya 38 akimalizia pasi ya Geny Catamo.
Msumbiji sasa inahitaji pointi tatu katika mechi zake mbili zilizobakia dhidi ya Senegal na Sudan ili nayo ijihakikishie tiketi ya kushiriki AFCON 2027.
Ethiopia nayo ina nafasi kama itazifunga Senegal na Sudan kisha kuombea Msumbiji ifanye vibaya.
Jijini Nairobi, wenyeji Kenya wamepoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini.
Mabao ya wageni yamefungwa na Relebohile Mofokeng huku la Kenya likifungwa na Mohamed Bajaber.