Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo azuiwa kwenda Uzbekistan

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioachwa na kocha Ange Postecoglou katika kikosi kilichosafiri kwenda Tashkent kwa mchezo wa Jumatatu.

TASHKENT, UZBEKISTAN: NYOTA wa Al Nassr na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amekosa safari ya timu yake kwenda Uzbekistan kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Asia dhidi ya Pakhtakor, huku kukiwa na taarifa za wasiwasi wa kiusalama unaoendelea katika eneo hilo.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioachwa na kocha Ange Postecoglou katika kikosi kilichosafiri kwenda Tashkent kwa mchezo wa Jumatatu.

Hata hivyo, kutokuwepo kwa mshambuliaji huyo hakukuwa kikwazo kwa Al Nassr, ambayo iliibuka na ushindi mkubwa wa mabao 6-2.

RONA 01

Kiungo mshambuliaji wa Ureno, Joao Felix, ndiye aliyeibeba timu hiyo kwa kufunga mabao mawili katika ushindi huo.

Kocha Postecoglou pia aliwapumzisha Kingsley Coman na Mohamed Simakan, akieleza kuwa alifanya hivyo kutokana na wingi wa michezo na safari ndefu zinazowakabili wachezaji wake.

Uamuzi huo umekuja wiki moja baada ya mchezo wa Al Nassr dhidi ya Al Wasl kuahirishwa, kufuatia klabu hiyo ya Falme za Kiarabu kukataa kusafiri kutokana na hali ya kiusalama katika eneo la Saudi Arabia.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa baadhi ya viwanja vya ndege nchini Saudi Arabia vimekuwa vikikabiliwa na mashambulizi yanayohusishwa na waasi wa Kihouthi, ambao wanatajwa kuungwa mkono na Iran.

RONA 03

Mashambulizi hayo yameongeza wasiwasi kuhusu usalama katika eneo hilo, huku ripoti zikieleza kuwa shambulizi moja la hivi karibuni lilisababisha vifo vya watu 13.

Licha ya kukosa mchezo huo, Ronaldo anaendelea kuwa kwenye kiwango kizuri cha ufungaji baada ya wiki iliyopita kupachika mabao matatu katika ushindi dhidi ya Al Kholood kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Hat-trick hiyo ilimfikisha kwenye mabao tisa katika mechi 12 alizokuwa amecheza msimu huu, huku idadi ya mabao yake katika maisha ya soka ikifikia 985.

Hiyo ina maana kuwa supastaa huyo anasogea kwa kasi kuelekea kufikisha mabao 1,000, rekodi ambayo amekuwa akiitamani kwa miaka kadhaa.

Akizungumza kuhusu ndoto hiyo katika mahojiano na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Manchester United, Rio Ferdinand, mwaka 2024, Ronaldo amesema:

RONA 02

"Nataka kufikisha mabao 1,000. Kama sitapata majeraha, hilo ndilo jambo muhimu zaidi kwangu. Kwanza nilitaka kufikisha mabao 900, sasa changamoto yangu ni kufikisha 1,000."

Mbali na mafanikio ya uwanjani, Ronaldo pia ameendelea kutengeneza historia nje ya uwanja.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, nyota huyo alitajwa kuwa mwanasoka wa kwanza kufikia hadhi ya kuwa bilionea, kutokana na mapato yake makubwa ya mishahara, matangazo ya kibiashara na uwekezaji.

Inaripotiwa kuwa mshahara wake Al Nassr unakadiriwa kufikia Pauni 488,000 kwa siku, huku mapato yake ya kibiashara nje ya uwanja yakitajwa kufikia pauni milioni 42 kwa mwaka.