Rashford mambo si mambo Barcelona
Muktasari:
- Winga huyo wa Manchester United aliyejiunga na Barcelona kwa mkopo alitokea benchi kwenye mechi ya kwanza ya La Liga wiki iliyopita na kufanya vizuri dhidi ya Real Mallorca, lakini wiki moja baadaye, staa huyo amekumbana na nyakati mbaya kabisa wakati alipotewa uwanjani kipindi cha kwanza na mashabiki kumsakama kwa kiwango chake.
BARCELONA, HISPANIA: STAA Marcus Rashford amekutana na wakati mgumu katika mechi yake aliyoanzishwa kwa mara ya kwanza na Barcelona kwenye La Liga baada ya kutolewa kipindi cha kwanza huku timu hiyo ikiwa nyuma kwa mabao 2-0 mbele ya Levante na mashabiki wakimkosoa.
Winga huyo wa Manchester United aliyejiunga na Barcelona kwa mkopo alitokea benchi kwenye mechi ya kwanza ya La Liga wiki iliyopita na kufanya vizuri dhidi ya Real Mallorca, lakini wiki moja baadaye, staa huyo amekumbana na nyakati mbaya kabisa wakati alipotewa uwanjani kipindi cha kwanza na mashabiki kumsakama kwa kiwango chake.
Kocha Hansi Flick alimtoa Rashford kipindi cha kwanza sambamba na Marc Casado. Dani Olmo na Gavi waliingizwa kuchukua nafasi na hatimaye Barcelona ilifanikiwa kupindua meza na kushinda mechi hiyo 3-2.
Pedri alihitaji dakika nne tu kwenye kipindi cha pili kufunga bao la kwanza la Barcelona kabla ya Ferran Torres kusawazisha. Barcelona ilipata ushindi kwenye dakika za majeruhi baada ya beki wa Levante, Unai Elgezabal kujifunga kwa kichwa wakati alipokuwa akijaribu kuokoa krosi ya Lamine Yamal.
Rashford sasa atalazimika kujitathmini sana ubora wake kutokana na kocha Flick kuwa na utajiri mkubwa wa wachezaji kwenye safu ya ushambuliaji.
Shabiki mmoja alisema: “Rashford amefanikiwa kuleta akili ya Man United hapa Barca.” Mwingine aliandika: “Unaweza kumwondoa Rashford nje ya Man United, lakini huwezi kuitoa Man United nje ya Rashford.”
Flick hakutaka kumpa lawama Rashford kwa kucheza kwa kiwango cha chini kwenye kipindi cha kwanza, akiamini mchango wa staa huyo utaonekana kwa mechi zijazo katika msimu huu