Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majirani Kenya waanza kwa kichapo WAFCON

Muktasari:

  • Wenyeji hao walianza kuonyesha ubora tangu fimbi ya mwamuzi ilipopulizwa kwa kufungua akaunti ya mabao kupitia kwa Sakina Ouzraoui aliyefunga dakika ya 19 kabla ya Maryame Atiq Ez-Zity kuongeza bao la pili dakika ya 28.

Morocco imeanza vyema kampeni ya kutetea heshima nyumbani baada ya kuichapa Kenya kwa mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026) uliopigwa katika Uwanja wa Moulay El Hassan, Rabat.

Wenyeji hao walianza kuonyesha ubora tangu fimbi ya mwamuzi ilipopulizwa kwa kufungua akaunti ya mabao kupitia kwa Sakina Ouzraoui aliyefunga dakika ya 19 kabla ya Maryame Atiq Ez-Zity kuongeza bao la pili dakika ya 28.

Kenya ilijikuta ikizidiwa kasi na ubora wa wapinzani wao, huku safu ya ulinzi ikishindwa kuhimili mashambulizi ya mara kwa mara ya Morocco.

Mshambuliaji Ibtissam Jraïdi aliihakikishia Morocco ushindi mnono baada ya kufunga mabao mawili, la kwanza dakika ya 32 na la pili dakika ya 47, na kufikisha mabao manne yaliyoizamisha Harambee Starlets.

Baada ya bao hilo la nne, Morocco iliendelea kumiliki mchezo huku ikitengeneza nafasi nyingine kadhaa, lakini kipa wa Kenya, Lilian Awuor, aliokoa mashambulizi mengi kwa timu yake.

Takwimu za mchezo zinaonyesha wenyeji walimiliki mpira kwa asilimia 64.7 dhidi ya asilimia 35.3 za Kenya, wakipiga mashuti 19 huku 10 yakilenga lango.

Kenya ilipiga mashuti nane, matatu kati ya hayo yakilenga lango, ishara ya ugumu walioupata kupenya safu ya ulinzi ya Morocco.

Mshambuliaji wa Kenya, Tereza Engesha alijaribu kuisumbua Morocco kwa mashuti mawili yaliyolenga lango, lakini juhudi zake hazikutosha kuivusha timu hiyo.

Licha ya kupoteza kwa mabao manne, kipa Awuor alikuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha ushindani mkubwa kwa Kenya baada ya kuokoa mipira sita ya hatari, huku Morocco ikilazimisha mashambulizi mengi langoni mwao.

Kenya pia ilifanya makosa 17 dhidi ya 11 ya Morocco na kuonyeshwa kadi moja ya njano, jambo lililoonyesha ilivyokuwa ikihangaika kuzuia kasi ya wapinzani wake.