Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Trump kuhudhuria hafla ya upangaji makundi Kombe la Dunia 2026

TRUMP Pict

Muktasari:

  • Kombe la Dunia limepewa umuhimu mkubwa katika utawala wa Trump pamoja na sherehe za miaka 250 ya uhuru wa Marekani.

Ikulu ya Marekani imethibitisha kwamba, Rais Trump atahudhuria hafla ya droo ya upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia 2026, itakayofanyika mjini Washington mwishoni mwa wiki hii. Marekani itashiriki fainali hizo kama mwenyeji pamoja na Canada na Mexico.

“Ijumaa hii, Rais Trump atahudhuria hafla ya droo ya upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia kwenye ukumbi wa Kennedy Center,” amesema Katibu wa Habari wa Ikulu, Karoline Leavitt, katika mkutano na waandishi wa habari.

Kombe la Dunia limepewa umuhimu mkubwa katika utawala wa Trump pamoja na sherehe za miaka 250 ya uhuru wa Marekani.

Hata hivyo, tukio hilo kubwa la michezo halijakwepa matatizo ya kisiasa kutokana na msimamo mkali wa Trump katika masuala kadhaa.

TR 01

Trump, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republican, ametoa uwezekano wa kuhamisha baadhi ya mechi kutoka baadhi ya miji mwenyeji ndani ya Marekani kutokana na hatua za kudhibiti uhalifu na uhamiaji haramu katika maeneo ambayo yanaendeshwa na chama cha Democratic.

Droo ya upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia 2026 itahusisha timu shiriki 48 ambazo zitawekwa katika makundi ili kuamua nani atacheza na nani katika hatua ya awali ya mashindano hayo. 

Timu hizo 48 zitagawanywa katika vyungu vinne. Chungu cha kwanza kitajumuisha timu tatu mwenyeji pamoja na timu tisa zenye viwango vya juu zaidi duniani, kama Brazil, Argentina, Ufaransa, Hispania, Uingereza, Ujerumani, na nyingine. 

TR 02

Chungu cha pili, tatu na nne kitajumuisha timu zilizobaki kulingana na viwango vyao vya mashindano, ikiwemo nafasi chache zinazopatikana kupitia michezo ya mchujo (play‑offs).

Utaratibu wa droo ni kwamba timu za chungu cha kwanza zitapangwa kwenye makundi (kundi A hadi L), huku timu za chungu cha pili, tatu na nne zikivutwa moja baada ya nyingine ili kujaza makundi. 

Kuna kanuni za kuepuka makundi yenye timu kutoka bara moja, isipokuwa UEFA ambapo kundi linaweza kuwa na timu moja au mbili za Ulaya, lakini si zaidi ya hizo.