Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Promota Frank Warren afichua Tyson Fury kurudi ulingoni

TYSON Pict

Muktasari:

  • Fury, anayefahamika kama “The Gypsy King”, alitangaza kustaafu masumbwi Januari 2025 baada ya kupoteza mapambano mawili mfululizo dhidi ya bondia wa Ukraine, Oleksandr Usyk.

Promota wa masumbwi, Frank Warren, amethibitisha kuwa bingwa wa zamani wa uzani wa juu, Tyson Fury, anapanga kurejea ulingoni 2026.

Fury, anayefahamika kama “The Gypsy King”, alitangaza kustaafu masumbwi Januari 2025 baada ya kupoteza mapambano mawili mfululizo dhidi ya bondia wa Ukraine, Oleksandr Usyk.

Warren, mwenye umri wa miaka 73, amethibitisha kuwa Fury anapanga kurudi ulingoni, akiwa na mipango na malengo tofauti na aliyokuwa nayo kabla ya kutangaza kustaafu.

“Nilizungumza naye wiki iliyopita. Aliniambia kwamba anataka kurudi kupigana mwaka ujao. Anataka kufanya hivyo. Mwaka huu amechoka kwa mambo mengi. Hajapigana mwaka huu, lakini kama tulivyoona sote, alikuwa akitengeneza filamu ya maisha yake.

TY 03

"Amefanya kazi na Netflix kwenye mfululizo wa ‘At Home with the Furys’. Pia ana makala nyingine ya maisha yake ambayo anakamilisha, pamoja na mambo mengine. Lakini amenihakikishia moja kwa moja kuwa anataka kupigana tena mwaka ujao. Kwa hiyo tutakaa chini na kuona." amesema Warren.

Fury tayari amedokeza kurudi kwake ulingoni kunawezekana, huku akiendelea kujiweka fiti licha ya kuwa amestaafu.

Julai 2025 alisema: “Namemisi masumbwi, kila siku ninapoamka asubuhi ninamisi mchezo huu ninaoupenda. Nimekuwa mbali kwa miezi saba, ninamisi kila siku. Kwa sasa niko wazi kupokea ofa.

"Mwaka ujao The big GK (Gypsy King) atarudi kwa kishindo! Nitakuwa na miaka 37 ndani ya wiki tatu, nitakuwa ‘mzee wa kazi’ huku vijana wakija juu, itakuwa ngumu!"

TY 02

Tangu Furry kupoteza dhidi ya Usyk mwenye miaka 38, mpinzani wake huyo ameendelea kung’ara, ikiwa ni pamoja na kumshinda bondia chipukizi Daniel Dubois, mwenye miaka 28.

Bondia mwingine wa Kiingereza, Fabio Wardley (30), naye ameanza kujitokeza katika nafasi za juu za uzani wa juu mwaka huu, huku Moses Itauma (20) akiendeleza mwelekeo wake kuelekea taji la dunia kwa kumshinda Dillian Whyte Agosti 2025.

Hata hivyo, pambano linalozungumziwa zaidi kwa sasa kwa upande wa Fury ni lile la muda mrefu linalosubiriwa dhidi ya mpinzani wake mkubwa, Anthony Joshua.

Ingawa mvuto wa pambano hilo umepungua kidogo kutokana na kuporomoka kwa viwango vya wote wawili kwa sasa, mashabiki wengi bado wangetamani kuliona likitokea, ikiwa kama jibu la moja ya maswali makubwa zaidi katika historia ya ngumi za uzani wa juu: "Nani bora kati yao?"

TY 01

Kwa upande wa Joshua, naye anatajwa huenda akapambana na Deontay Wilder katika Uwanja wa Wembley au na Martin Bakole barani Afrika, mwaka 2026.