Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pochettino atua Carrington, Kuanza kazi Man United

Muktasari:

  • Pochettino, mwenye umri wa miaka 54, aliagana na timu ya taifa ya Marekani (USMNT) baada ya kuiongoza kupata ushindi mnono wa jumla ya mabao 8-0 dhidi ya Haiti katika mechi zao za wiki hii.

LONDON, England: KOCHA mpya wa Manchester United, Mauricio Pochettino ameanza rasmi majukumu yake baada ya kuonekana akiwasili katika kituo cha mazoezi cha klabu hiyo, Carrington, Jumatano asubuhi.

Pochettino, mwenye umri wa miaka 54, aliagana na timu ya taifa ya Marekani (USMNT) baada ya kuiongoza kupata ushindi mnono wa jumla ya mabao 8-0 dhidi ya Haiti katika mechi zao za wiki hii.

Sasa anajiandaa kukabiliana na jukumu kubwa la kuijenga upya Manchester United, ambayo imekuwa katika hali mbaya na kushuka hadi eneo la hatari ya kushuka daraja.

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na Chelsea alikubali kuiongoza United wiki iliyopita, baada ya Michael Carrick kutimuliwa kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo, iliyopata ushindi mmoja pekee katika Ligi Kuu England msimu huu.

Pochettino anakabiliwa na mtihani mgumu katika mchezo wake wa kwanza, ambapo United itasafiri kukabiliana na wapinzani wao Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili.

Kocha huyo alionekana akiwasili Carrington Jumatano asubuhi kuanza kazi, saa chache baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Manchester kwa ndege binafsi aina ya Gulfstream G700 yenye thamani ya pauni milioni 70.

Amebakiwa na siku chache tu za kuiandaa timu yake kabla ya safari ya Anfield.

Pochettino ameungana na makocha wake wa kawaida, Jesus Perez, Miguel D’Agostino na Toni Jimenez, ambaye ni kocha wa makipa. Mwanaye, Sebastiano, anayefanya kazi ya sayansi ya michezo, pia atakuwa sehemu ya benchi lake la ufundi.

Aidha, anatarajiwa kumwajiri Silvia Tuya kuwa kocha wa nguvu na mazoezi ya viungo, hatua itakayomfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuingia katika benchi la ufundi la Manchester United. Tuya aliwahi kufanya kazi na Pochettino katika timu ya taifa ya Marekani.

Perez, Jimenez na Sebastiano wamekuwa Manchester tangu Jumapili kuanza maandalizi ya awali, huku D’Agostino na Tuya wakibaki Marekani pamoja na Pochettino kusimamia mchezo wa mwisho dhidi ya Haiti.