Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pesa juu ya pesa, Shakira akiandika historia Copa America

Muktasari:

  • Haitakuwa fainali ya kinyonge. Haijalishi nani kapigwa lakini mashabiki zaidi ya 65000 watapata burudani tamu kutoka kwa mwanamama Shakira.

MIAMI, MAREKANI: USIKU wa kuamkia kesho, Jiji la Miami litasimama kwa muda kupisha fainali ya wakali wawili, Argentina dhidi ya Colombia kwenye Uwanja wa Hard Rock.

Haitakuwa fainali ya kinyonge. Haijalishi nani kapigwa lakini mashabiki zaidi ya 65000 watapata burudani tamu kutoka kwa mwanamama Shakira.

Shoo hiyo ataifanya wakati wa mapumziko ya mchezo huo na kwa majira ya Afrika Mashariki utapigwa saa 9:00 usiku.

Tukio hilo ni mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo na mara nyingi wasanii walifanya shoo kabla ya mchezo na inakuwa ni rekodi kwa Shakira ambaye mbali na tukio hilo anatarajiwa kupiga mkwanja wa maana.

Mrembo huyu mwenye umri wa miaka 47 kwa mkwanja atakaopiga ataendelea kuishi maisha ya kishua. Hivi ndivyo anavyopiga mkwanja wake na huu hapa utajiri wake.


ANAPIGAJE PESA?

Ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 300 milioni na kwa kiasi kikubwa kipato chake kinatokana na muziki. Nyimbo zake, Waka Waka (It’s Time For Africa),  Chantaje na Loca zimemwingizia pesa nyingi kutokana na mauzo yake.

Hadi kufikia mwaka 2024, Waka Waka pekee iliuzwa mara milioni 10 kwenye mitandao wa Spotify, Apple Music, mbali ya Youtube. Hadi sasa ameuza kopi milioni 10 za kazi zake.

Pia anaingiza pesa nyingine kutokana na kazi ya ujaji na kufundisha muziki katika mashindano mbalimbali na kwa mwaka anapata Dola 12 milioni.

Mwaka 2021 aliuza haki ya usambazaji wa baadhi ya nyimbo zake kwenda Kampuni ya Hipgnosis Songs Fund na inadaiwa alipata zaidi ya Dola 100 milioni.

Pesa nyingine anapata kutokana na shoo mbalimbali anazofanya katika matamasha kama El Dorado World Tour, Oral Fixation World Tour na Tour of the Mongoose, ambayo amekuwa akiyafanya kila mwaka na pesa anayolipwa inakadiriwa ni kati ya Dola 1 hadi 5 milioni kwa tamasha moja pekee.

Kwa mujibu wa jarida la  Forbes, kupitia Youtube wimbo aliomshirikisha Rauw Alejandro 'Te Felicito' ulimwingizia Dola 13.6 milioni hadi kufikia Aprili  2022, pia 'Monotonía', aliomshirikisha Ozuna ulimwingizia Dola 4.9 milioni.

Pia anaingiza pesa kwa kazi yake ya ubalozi wa kampuni mbalimbali kama Activia, Burberry, Crest 3D White na Epson EpiqVision.


MJENGO

Mwaka 2018, aliiuza nyumba yake iliyokuwa huko Miami kwa Dola 11.6 milioni na una upana wa futi 20,726, wenye vyumba sita vya kulaa pamoja na vyoo saba.

Mjengo huo uko mtaa wanakoishi mastaa wengine kama Damon, Ricky Martin, Jennifer MattLopez, Alex Rodriguez na Michael Bay.

Baada ya kuachana na Pique mwaka 2022, waliweka sokoni nyumba yao iliyopo Barcelona na Shakira na watoto wake wakaenda Marekani ambako inadaiwa amepanga nyumba maeneo ya Miami yenye thamani ya Dola 15 milioni.

Vilevile imeripotiwa yupo katika harakati za kujenga nyumba mpya itakayokuwa na thamani ya Dola 50 milioni.


NDINGA

Ana magari kibao ya thamani kubwa kama;

Mercedes S-Class - Dola 125,000,

Mercedes SL550 - Dola 114,700.

Audi A7 Sportback, Mercedes SLK250, Tesla Model S, BMW X6, Audi Q7, Jeep Wrangler na Mini Cooper


MSAADA KWA JAMII

Anamiliki taasisi yake mwenyewe iitwayo Fundacion Piesdescalzos ambayo imejikita katika kutoa misaada mbalimbali duniani.

Misaada hiyo imejikita katika elimu na maendeleo ya jamii.

Taasisi hii imekuwa ikijenga shule katika nchi mbalimbali pamoja na kusaidia kujenga miundombinu kama visima.


MAISHA NA BATA

Alikuwa katika uhusiano na mchezaji wa zamani wa Barcelona Gerrard Pique aliyeachana naye mwaka 2022. Katika kipindi chote walichodumu wawili hawa walipata watoto wawili. Walianzisha uhusiano mwaka 2010 baada ya kukutana katika fainali za Kombe la Dunia.