Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Perez, Riquelme wachuana Vikali, Mourinho na Haaland watajwa

MAKONDA Pict

Muktasari:

  • Jose Mourinho na Erling Haaland ni baadhi ya majina makubwa yaliyotumika kuhamasisha kampeni za rais wa sasa Florentino Perez na mpinzani wake, Enrique Riquelme.

MADRID, HISPANIA: MIVUTANO ya kisiasa ndani ya Real Madrid imeanza kuchomoza huku uchaguzi wa rais wa klabu hiyo ukikaribia Jumapili hii.

Jose Mourinho na Erling Haaland ni baadhi ya majina makubwa yaliyotumika kuhamasisha kampeni za rais wa sasa Florentino Perez na mpinzani wake, Enrique Riquelme.

Wapigakura wa Real Madrid wanapaswa kuchagua kati ya Perez mwenye umri wa miaka 79 na mpinzani wake mwenye miaka 37 na kila mmoja ameahidi mambo makubwa ikiwa atachaguliwa kuongoza klabu.

Perez, aliyekuwa kwenye uongozi wa Madrid tangu 2009, ameamua kumpa Mourinho kipindi cha pili kuifundisha timu, baada ya kocha huyo raia wa Ureno kuwa kiongozi wa Los Blancos kati ya 2010 na 2013.

Hata hivyo, uhamisho wake kutoka Benfica kwenda Bernabeu bado haujatangazwa rasmi na utategemea kama bosi huyo atashinda.

Hata hivyo, ukurasa rasmi wa kampeni za Perez kwenye mitandao ya kijamii ulionyesha video Jumatano usiku ukiwa na kichwa cha habari:

“Historia kubwa kuandikwa” ambapo Mourinho aliibuka katikati. Video hiyo ilijumuisha maneno: “Wakati kwenye TV wanazungumza, na kuzungumza.” Taarifa hiyo ilitoka wakati ambapo mshindani wake anapiga kampeni kwenye televisheni.

MAN 01

Mkataba mpya wa Mourinho unaaminika utakwenda hadi majira ya joto ya 2028, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, ambaye hajashinda ligi kwa miaka 11, atajiunga na klabu inayokabiliwa na changamoto baada ya msimu uliopita kujaa migogoro kati ya wachezaji, kutoka mapema kwenye Ligi ya Mabingwa, na Barcelona ikitwaa taji la LaLiga.

Perez, ambaye amekuwa rafiki wa Mourinho tangu alipoondoka Bernabeu, ameahidi kutangaza usajili wake mkubwa wa kwanza Alhamisi. Wachezaji wanaotarajiwa kujiunga ni pamoja na kiungo wa zamani wa Liverpool Ibrahima Konate na beki wa kulia wa Uholanzi Denzel Dumfries lakini yote ikielezwa yatafanyika endapo atashinda.

Hadi sasa Perez hajakumbana na ushindani katika uchaguzi wa awamu tano zilizopita, lakini safari hii amekabiliana na Riquelme ambaye anaonekana kupata uungwaji mkono mkubwa.

Riquelme, amekuwa akiahidi mabadiliko makubwa na kuahidi kutompa mkataba Mourinho:

“Ikiwa nitashinda uchaguzi, nitaleta kocha bingwa Real Madrid. Kocha mkubwa zaidi unayeweza kufikiria. Jose Mourinho si kocha wetu. Tutapata kocha anayependwa kweli na mashabiki wote wa Madrid.”

Ingawa hajafichua kocha wake, Riquelme ametoa ahadi ya kumfanya gwiji wa zamani wa timu hiyo, Raul, kuwa mkurugenzi wake wa michezo ikiwa atachaguliwa. Pia ameiahidi klabu kuwa atasaini nyota wa Hispania na kiungo wa sasa wa Manchester City, Rodri, pamoja na staa wa City, Erling Haaland, huku akichapisha jezi ya Madrid yenye jina la Haaland mgongoni kwenye kampeni zake za televisheni.

MAN 02

Mourinho bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Benfica, na kwa vile kifungu chake cha kuachwa kimeisha, Madrid italazimika kulipa zaidi ya pauni 12 milioni kama fidia, kulingana na ripoti.

Majira ya joto yanatarajiwa kuwa ya mabadiliko makubwa Santiago Bernabeu, huku Mourinho akikosa msaada wa Alvaro Arbeloa. Arbeloa, ambaye amefundisha timu tangu Januari, amethibitisha hatabaki chini ya Mourinho:

“Mourinho ana kikosi bora cha ufundi, amezungukwa na watu wazuri. Akija, ataleta timu yake, kama inavyostahili. Sioni nafasi yangu kujiunga naye. Nimechukua muda wa miezi minne kuipambania Madrid. Sasa ni wakati wa kujizingatia mimi mwenyewe. Nimechukua hatua na niko tayari kwa changamoto mpya.”