Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nunez aingia anga za Napoli, Liverpool ikipokea ofa ya Al Nassr

TETESI Pict

Muktasari:

  • Ripoti kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya England zinadai kwamba Liverpool ipo tayari kumuuza Nunez na imepokea ofa nono kutoka Al Nassr ya Saudia, hata hivyo mchezaji mwenyewe bado anataka kuendelea kucheza soka la kiushindani, hivyo angependa kujiunga na timu ya Ulaya kama atauzwa.

NAPOLI inakumbana na upinzani mkali kutoka timu za Saudi Arabia katika mpango wake wa kutaka kumsajilj straika wa Liverpool na timu ya taifa ya Uruguay, Darwin Nunez.

Ripoti kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya England zinadai kwamba Liverpool ipo tayari kumuuza Nunez na imepokea ofa nono kutoka Al Nassr ya Saudia, hata hivyo mchezaji mwenyewe bado anataka kuendelea kucheza soka la kiushindani, hivyo angependa kujiunga na timu ya Ulaya kama atauzwa.

Liverpool ambayo ipo karibu kumsajili Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen, inataka kutumia kiasi cha pesa itakachopata kwenye dili la Nunez kuongezea kwenye ada ya uhamisho wa fundi huyo.

Nunez mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 47 za michuano yote, akafunga mabao saba na kutoa asisti saba.


Joao Pedro

NEWCASTLE imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Brighton & Hove Albion ili kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na Brazil, Joao Pedro, 23, baada ya mchezaji mwenyewe kuwaambia wawakilishi wake kwamba angependa kujiunga na vigogo hao.

Mkataba wa sasa wa Pedro unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


James McAtee

BAYER Leverkusen inajiandaa kuwasilisha ofa rasmi kwenda Manchester City kwa ajili ya kumsajili kiungo wao raia wa England, James McAtee, 22, mara baada ya dirisha la usajili litakapofunguliwa kuanzia kesho Jumatatu Juni 16 hadi Septemba 1.

James ambaye anaripotiwa kuwa anaweza kuuzwa kwa zaidi ya Pauni 30 milioni, mkataba wake na Man City unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Kyle Walker

KOCHA Jose Mourinho anayeifundisha Fenerbahce amewasilisha jina la beki wa kulia wa Manchester City,  Kyle Walker, 35, akitaka asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Walker ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo AC Milan, ameambiwa atafute timu ya kujiunga nayo kwani Man City haina mpango wa kumrudisha tena kikosini, licha ya kuonekana kufanya vizuri Milan aliko kwa mkopo.


Fred

EVERTON inataka kumsajili kiungo wa zamani wa  Manchester United, Mbrazili Fred, 32 ambaye kwa sasa anaichezea Fenerbahce ya Uturuki.

Staa huyu ameivutia sana Everton kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu alipojiunga na Fenerbahce baada ya kuachana na Manchester United mwaka 2027.

Katika msimu uliopita alicheza mechi 45 za michuano yote.


Ilkay Gundogan

BAADA ya kukamilisha usajili wa winga wa zamani wa Bayern Munich na Ujerumani, Leroy Sane  kwa usajili huru, mabosi wa Galatasaray sasa wanadaiwa kuwa wamekutana na wawakilishi wa kiungo wa Manchester City, Ilkay Gundogan, 34, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kuipata saini yake katika dirisha hili. Galatasaray inapambana kusajili wachezaji bora ili kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.


Mahamadou Sangare

MANCHESTER City ipo katika mchakato wa kutaka kumsajili straika wa ParisSaint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Mahamadou Sangare, 18, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza kwamba PSG iko tayari kutoa karibia Pauni 30 milioni ili kunasa huduma yake na atasaini mkataba wa miaka mitano.


Ruben Loftus-Cheek

LAZIO inataka kumsajili kiungo wa AC Milan, Ruben Loftus-Cheek, 29, katika dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa ni pendekezo la kocha wake Maurizio Sarri ambaye alishawahi kumfundisha staa huyu walipokuwa Chelsea. Milan haionekani kuwa na mpango wa kumzuia Ruben ambaye hajaonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita.