Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neymar ampa ndege baada ya babake kuuawa

NEYMAR Pict

Muktasari:

  • Baada ya tukio hilo, Neymar aliingilia kati na kumruhusu Rony kutumia ndege yake binafsi ili yeye pamoja na familia yake waweze kusafiri kwenda jimbo la Para, ambako tukio hilo linadaiwa kutokea.

SAO PAOLO, BRAZIL: NYOTA wa Santos, Rony, amemshukuru mshambuliaji mwenzake Neymar kwa msaada na ukarimu aliomwonesha baada ya baba yake kufariki dunia kwa kuuawa.

Baba wa Rony, Marigerson Barbosa Carneiro mwenye umri wa miaka 72, aliuawa kwa kuchomwa kisu Jumatatu iliyopita.

Baada ya tukio hilo, Neymar aliingilia kati na kumruhusu Rony kutumia ndege yake binafsi ili yeye pamoja na familia yake waweze kusafiri kwenda jimbo la Para, ambako tukio hilo linadaiwa kutokea.

NEYM 01

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Marca, polisi wanaendelea kuchunguza mauaji hayo na tayari mwanamke mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Rony, mwenye umri wa miaka 31, aliweka picha yake akiwa na baba yake kupitia mtandao wa Instagram, akiambatanisha na ujumbe wa majonzi na kumshukuru Neymar pamoja na watu wengine waliompa pole na msaada katika kipindi hicho kigumu.

Katika ujumbe huo aliandika:

"Leo nimepokea moja ya taarifa ngumu zaidi katika maisha yangu, kifo cha baba yangu.

NEYM 02

"Ninakabiliana na wakati huu nikiwa na huzuni kubwa na moyo mzito, lakini bado nimeshikilia imani yangu, nikimtumaini Mungu kuwa ndiye chanzo cha nguvu zetu na kwamba atatupatia nguvu za kuvuka kipindi hiki kigumu.

"Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Santos, benchi la ufundi, hasa kocha Cuca, pamoja na kila mmoja aliyeonesha kujali, kuelewa na kutuunga mkono tangu alipopata taarifa hizi.

"Shukrani za pekee kwa Neymar kwa ukarimu wake na utayari wa kunikopesha ndege yake binafsi, jambo lililowezesha familia yangu kusafiri."

Neymar anamiliki ndege binafsi aina ya Dassault Falcon 900 LX, ambayo thamani yake inakadiriwa kufikia pauni37 milioni.

NEYM 03

Mshambuliaji huyo anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Brazil, anadaiwa kuwa na utajiri binafsi unaozidi pauni 300 milioni, alioupata kwa kiasi kikubwa kupitia mishahara mikubwa wakati akiichezea Barcelona, Paris Saint-Germain na Al-Hilal.