Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo, Messi waacha rekodi mpya

OBRIGADO Pict

Muktasari:

  • Ingawa Messi aliagwa katika sherehe maalumu iliyofanyika baadaye Oktoba 6, 2026 katika Uwanja wa Estadio Monumental mjini Buenos Aires, ambapo walishinda mabao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Benin, ameonekana kumshawishi na mwenzake, Ronaldo, kufuata nyayo zake. Messi ana umri wa miaka 39 huku Ronaldo akiwa na 41.

RIYADH, SAUDI ARABIA: JUZI, ulimwengu wa soka ulipokea taarifa ya mshtuko ya nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano ronaldo kutangaza kustaafu kuichezea baada ya kuitumikia kwa miaka 23 ikiwa ni takriban miezi mitatu baada ya mshindani wake mkuu, Lionel Messi kuagwa rasmi na Argentina Agosti 31, 2026.

Ingawa Messi aliagwa katika sherehe maalumu iliyofanyika baadaye Oktoba 6, 2026 katika Uwanja wa Estadio Monumental mjini Buenos Aires, ambapo walishinda mabao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Benin, ameonekana kumshawishi na mwenzake, Ronaldo, kufuata nyayo zake. Messi ana umri wa miaka 39 huku Ronaldo akiwa na 41.

Achana na hayo, huku nyuma nyota hao wameacha rekodi kibao ambazo kuiandika zinaweza kuchukua kurasa nyingi kumalizika. Hata hivyo kuna hii moja; ni gwiji gani amekosa penalti nyingi zaidi katika maisha yake ya soka?

Kuna nyakati chache katika maisha ya mchezaji wa soka zinazoweza kumletea presha kubwa kama kupiga penalti. Watu wengi wanaweza kufikiri kwamba kupiga mpira na kuuingiza wavuni bila kizuizi kutoka umbali wa mita 11 ni jambo rahisi, lakini hakuna shaka kuwa kufunga penalti kunahitaji uimara wa kisaikolojia pamoja na uwezo wa kiufundi. Hata wachezaji bora zaidi kuwahi kucheza soka wamewahi kukosa penalti wanapokuwa chini ya presha, kama inavyoonekana hapa chini.


CRISTIANO RONALDO

Kwa mujibu wa takwimu za Transfermarkt, hakuna mchezaji aliyekosa penalti nyingi zaidi katika mashindano yote tangu 2001 kuliko Cristiano Ronaldo. Sehemu ya mwisho ya maisha ya soka ya nyota huyo wa Ureno imejikita katika jitihada zake zisizokoma za kufunga mabao, huku uwezo wake wa kufunga penalti ukiwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo.

Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, Ronaldo amepiga penalti zisizopungua 196 akiwa na klabu na timu ya taifa katika mashindano yote.

Hiyo ni idadi kubwa kuliko mchezaji mwingine yeyote duniani. Na ingawa amefunga 167, pia amekosa 29. Kwa bahati mbaya, idadi hiyo pia ni kubwa kuliko ya mchezaji mwingine yeyote.


MESS 02

LIONEL MESSI

Ronaldo amekuwa akijitahidi kumzidi Lionel Messi katika kila kipengele, lakini huenda akasikitishwa kujua kwamba amemzidi pia katika suala hili. Messi amepiga penalti 121 katika kipindi hicho hicho, lakini amekosa 28. Ingawa kiwango cha Messi cha kufunga penalti ni cha chini kuliko cha Ronaldo, kikiwa asilimia 77 ikilinganishwa na asilimia 85 ya Ronaldo, idadi kubwa ya penalti alizopiga Ronaldo ndiyo inayomfanya kuwa mbele ya Messi na wachezaji wengine wote katika soka.


OBRI 01

HULK, TAVERNIER

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Givanildo Vieira de Sousa maarufu kama Hulk, anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo akiwa amekosa penalti mbili chini ya Messi. Hulk amekosa penalti 26 kati ya penalti 151 alizopiga katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Cha kushangaza, nafasi ya nne inashikiliwa na beki wa zamani wa Rangers, James Tavernier, ambaye amekosa penalti 22 kati ya 102 alizopiga.

Licha ya kuwa beki, mchezaji huyo wa England amekuwa akipenda kupiga penalti katika maisha yake ya soka na ana kiwango kizuri cha mafanikio cha asilimia 78.


OBRI 02

DUSAN, CAVANI

Dusan Tadic na Edinson Cavani wanashika nafasi ya tano kwa pamoja, baada ya kila mmoja kukosa penalti 19, ambapo Tadic amepiga penalti 104, huku Cavani akipiga penalti 81.


OBRI 03

NEYMAR, TOTTI NA ZAHAVI

Katika kukamilisha orodha ya wachezaji 10 bora, kuna majina mengine makubwa. Nyota wa zamani wa PSG, Neymar anashika nafasi ya saba pamoja na gwiji wa Roma, Francesco Totti, na Eran Zahavi. Kwa pamoja wote wamekosa penalti 18 katika kipindi hicho.

Nafasi ya 10 inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Italia, Ciro Immobile, ambaye amekosa penalti 17 kati ya penalti 91 alizopiga.

Naye Zlatan Ibrahimovic, kwa upande mwingine, anafurahi kujua kwamba penalti zake alizokosa hazijamuweka ndani ya orodha ya wachezaji 10 bora, ambapo mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Sweden amekosa penalti 16 kati ya 98 alizopiga, hivyo anashika nafasi ya 11.