Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli yajitupa kwa Kevin de Bruyne

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Awali, De Bruyne alihusishwa kuwa angetimkia kati ya Saudi Arabia au Marekani ambako kote kuna timu zilizohitaji kumsajili kwa ofa nono.

KIUNGO wa kati wa Manchester City, Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, yuko mbioni kukamilisha uhamisho wa kujiunga na mabingwa wa Serie A, Napoli, ndani ya wiki mbili zijazo.

Awali, De Bruyne alihusishwa kuwa angetimkia kati ya Saudi Arabia au Marekani ambako kote kuna timu zilizohitaji kumsajili kwa ofa nono.

Hata hivyo, kiungo huyu wa kimataifa wa Ubelgiji alikataa kwani anaamini bado ana nguvu za kucheza soka la kiushindani.

Mkataba wake na Man City unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, hivyo Napoli itamsajili akiwa mchezaji huru. Licha ya kuripotiwa kufikia hatua nzuri katika mchakato wao, bado hakuna uhakika wa asilimia mia kwa Napoli kumpata kwani timu nyingine pia zimeendelea kupambania saini yake. Msimu uliopita kiungo huyu alicheza mechi 39 za michuano yote.


Eberechi Eze

BAYERN Munich imehamishia nguvu zake kwa kiungo wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Eberechi Eze, mwenye umri wa miaka 26, baada ya kuikosa saini ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz ambaye amefikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mkataba wa Eze unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Mbali ya Newcastle, saini ya staa huyu pia inahitajika na Chelsea na Manchester United.


Kaoru Mitoma

MABOSI wa Bayern Munich, wanaendelea kufanya mazungumzo na Brighton kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa timu hiyo na Japan, Kaoru Mitoma, 28, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mbali ya Mitoma, mabosi wa Bayern pia wanafanya mazungumzo na AC Milan kwa ajili ya kuipata huduma ya Rafael Leao. Mkataba wa Mitoma unamalizika mwaka 2027.


Joao Pedro

LIVERPOOL na Newcastle zinatarajiwa kuingia katika vita ya kumsajili mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Brazil wa Brighton, Joao Pedro, mwenye umri wa miaka 23.

Pedro ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Brighton, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.


Luka Modric

INTER Milan inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Real Madrid, Luka Modric, mwenye umri wa miaka 39 baada ya staa huyo raia wa Croatia kuthibitisha kuwa ataondoka Real Madrid mwisho wa msimu.

Luka ambaye anawindwa pia na matajiri wa Saudi Arabia, msimu huu amecheza mechi 56 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Leroy Sane

GALATASARAY imewasilisha ofa kwa wawakilishi wa winga wa Bayern Munich na Ujerumani, Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 29, ambaye mkataba wake na Bayern unamalizika mwisho wa msimu huu.

Mbali ya Galatasaray staa huyu anahusishwa na vigogo wa ligi kubwa barani Ulaya kuanzia Hispania, England na Italia. Hata hivyo, hadi sasa bado hajafanya uamuzi wowote.


Nahuel Molina

NEWCASTLE ina matumaini ya kuzipiku Napoli, Juventus na Roma kwenye vita ya kuiwania saini ya beki wa kulia wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Nahuel Molina, mwenye umri wa miaka 27.

Molina ambaye ameonyesha kiwango bora kwa msimu huu, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 42.


Jarell Quansah

NOTTINGHAM Forest imepanga kumsajili beki wa Liverpool na England, Jarell Quansah, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Quansah ni miongoni mwa mastaa ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Liverpool na ameoyesha nia ya kuwa tayari kuondoka kwa mabingwa hao wa EPL.