Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nane Afrika zatinga 32 bora Kombe la Dunia U17

Muktasari:

  • Timu zilizofanikiwa kusonga mbele ni Misri, Mali, Uganda, Msumbiji, Ivory Coast, Senegal, Algeria na Morocco, huku Tanzania na Cameroon zikiaga mashindano hayo.

DOHA, Qatar: TIMU nane kati ya 10 zinazowakilisha Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 17 (U17) za mwaka 2026 zimefanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora baada ya kukamilika kwa michezo ya hatua ya makundi iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Timu zilizofanikiwa kusonga mbele ni Misri, Mali, Uganda, Msumbiji, Ivory Coast, Senegal, Algeria na Morocco, huku Tanzania na Cameroon zikiaga mashindano hayo.

Mali imekuwa timu bora zaidi ya Afrika katika hatua ya makundi baada ya kumaliza ikiwa na alama zote tisa kutokana na ushindi katika michezo yake yote mitatu.

Mali 'Aiglonnets' ilianza kwa kuichapa New Zealand mabao 3-0, kabla ya kuifunga Ubelgiji 2-1 na Vietnam mabao 2-0, matokeo yaliyoifanya kumaliza kileleni mwa kundi lake.

Kwa upande mwingine, Misri, Ivory Coast na Algeria kila moja ilikusanya alama sita, huku Senegal ikifuzu ikiwa na alama tano.

Uganda, Msumbiji na Morocco nazo zilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kila moja kukusanya alama nne.

Msumbiji ilipata nafasi ya kusonga mbele kupitia utaratibu wa timu bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu, na hivyo kukamilisha idadi ya timu nane za Afrika zitakazoendelea na michuano hiyo.

Tanzania na Cameroon ndizo timu mbili za Afrika zilizotolewa katika hatua ya makundi.

Tanzania ilimaliza ikiwa na alama moja baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wake wa mwisho wa kundi.

Cameroon yenyewe ilipoteza michezo yote mitatu iliyocheza na kuwa miongoni mwa timu zilizokuwa na matokeo mabaya zaidi katika mashindano hayo.

Kwa mujibu wa mfumo wa mashindano hayo, timu 32 zitashindana kupata timu 16 bora, zikiwemo timu mbili za juu kutoka katika kila kundi kati ya makundi 12, pamoja na timu nane bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Mbali na timu nane za Afrika, nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Korea Kusini, Ugiriki, Uruguay, Italia, Hispania, Mexico, Venezuela, Serbia, Brazil, Colombia, Ufaransa, Saudi Arabia, Argentina, Ubelgiji, Croatia, Jamhuri ya Dominika, Ecuador, China, Tajikistan, Jamhuri ya Ireland, Japan, Chile na Uzbekistan.