Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msala wa Arsenal mechi zijazo

Muktasari:

  • Mikel Merino aliisawazishia Arsenal dakika 59, baada ya Chelsea kutangulia kwa bao la Trevoh Chalobah mapema kipindi cha pili. The Blues ilikuwa pungufu na wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo Moises Caicedo kutolewa kwa kadi nyekundu.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL na Chelsea imeshindikana kupata mbabe katika kipute chao cha Jumapili iliyopita kwenye Ligi Kuu England baada ya kutoka sare ya bao 1-1 uwanjani Stamford Bridge, matokeo yanayoiweka The Gunners kileleni kwa tofauti ya pointi tano.

Mikel Merino aliisawazishia Arsenal dakika 59, baada ya Chelsea kutangulia kwa bao la Trevoh Chalobah mapema kipindi cha pili. The Blues ilikuwa pungufu na wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo Moises Caicedo kutolewa kwa kadi nyekundu.

Matokeo hayo bado yanakifanya kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kuendelea kuongoza ligi baada ya mechi 13. Manchester City ipo nyuma kwa pointi tano baada ya ushindi wao wa mabao 3-2 dhidi ya Leeds United, Jumamosi, huku Chelsea ikiwa nyuma kwa pointi moja zaidi.

Wiki hii, Arsenal itashuka tena uwanjani kukipiga na Brentford uwanjani Emirates, Jumatano kabla ya kukabiliana na Aston Villa, Jumamosi.

Jambo hilo limefanya kuwapo na mvuto mkubwa wa kutazama mechi zijazo za Arsenal zipoje ukinganisha na wapinzani wanaowakaribia kwenye msimamo huo wa Ligi Kuu England hadi sasa.

Mechi tano za Man City; Fulham (ugenini), Sunderland (nyumbani), Crystal Palace (ugenini), West Ham (nyumbani), Nottingham Forest (ugenini).

Mechi tano za Chelsea; Leeds United (ugenini), Bournemouth (ugenini), Everton (nyumbani), Newcastle United (ugenini), Aston Villa (nyumbani).

Mechi tano za Aston Villa; Brighton (ugenini), Arsenal (nyumbani), West Ham (ugenini), Man United (ugenini), Chelsea (ugenini).

Mechi tano za Brighton; Aston Villa (nyumbani), West Ham (nyumbani), Liverpool (ugenini), Sunderland (nyumbani), Arsenal (ugenini).

Mechi tano za Sunderland; Liverpool (ugenini), Man City (ugenini), Newcastle (nyumbani), Brighton (ugenini), Leeds (nyumbani).