Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpira wa ‘mkono wa Mungu’ wauza Sh9 bilioni

MUNGU Pict

Muktasari:

  • Maradona alifunga bao hilo kwa kutumia mkono na kuipatia Argentina ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England katika mchezo wa robo fainali uliochezwa nchini Mexico 1986.

LONDON, ENGLAND: MPIRA uliotumika katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 1986 kati ya Argentina dhidi ya England na Diego Maradona kufunga bao maarufu la ‘Mkono wa Mungu’ umeuzwa kwa pauni2.5 milioni (sawa takribani Sh9.06 bilioni za Tanzania.

Maradona alifunga bao hilo kwa kutumia mkono na kuipatia Argentina ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England katika mchezo wa robo fainali uliochezwa nchini Mexico 1986.

Baada ya mchezo huo, Maradona aliwaambia waandishi wa habari kuwa bao hilo lilifungwa “kidogo kwa kichwa cha Maradona na kidogo kwa mkono wa Mungu.”

Katika mchezo huo huo, Maradona alifunga pia bao lililokuja kutajwa kuwa ‘Bao la Karne’, baada ya kuwapita wachezaji watano wa England kabla ya kumtungua kipa Peter Shilton.

MUNG 02

Mpira huo aina ya Adidas Azteca uliuzwa kwa pauni2.5 milioni, katika mnada ulioendeshwa na Heritage Auctions nchini Marekani mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo, thamani hiyo ilikuwa chini ya makadirio ya awali, kwani ulitarajiwa kuuzwa kwa karibu dola 10milioni.

Mtaalamu wa minada wa Heritage, Mike Provenzale, amesema kabla ya mnada huo: “Hiki ni kitu cha aina yake. Kwa hoja, ni moja ya vitu muhimu zaidi vya soka kuwahi kuwepo.”

Mwamuzi wa mchezo huo, Mtunisia Ali Bin Nasser, alichukua mpira huo baada ya filimbi ya mwisho na kuuhifadhi kwa zaidi ya miaka 30.

MUNG 01

Mwaka 2023, Bin Nasser alisaini barua kuthibitisha kuwa huo ndio ulikuwa mpira pekee uliotumika katika mchezo huo, jambo ambalo baadaye lilithibitishwa pia na wataalamu huru.

Bin Nasser aliwahi kuuuza mpira huo mwaka 2022 kwa pauni1.74 milioni .

Mmiliki mpya aliurudisha tena kwenye mnada mwaka 2023, lakini haukuuzwa baada ya zabuni kushindwa kufikia kiwango cha chini cha thamani kilichowekwa.

Jezi aliyovaa Maradona katika mchezo huo pia iliuzwa kwa rekodi ya pauni 7.1 milioni katika mnada uliofanyika mwaka 2022.