Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho amkingia kifua Mbappe

MOURINHO Pict

Muktasari:

  • Mbappe aliomba msamaha baada ya kusema kuwa picha ya kuchekesha iliyomfurahisha zaidi ilikuwa ile iliyounganisha uso wake na picha ya “dikteta wa China” aliyefanana na Mao Zedong, aliyefariki mwaka 1976.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema mara nyingi ni bora mtu kunyamaza kuliko kutoa kauli zinazoweza kuwaudhi wengine, akizungumzia mjadala ulioibuka baada ya mshambuliaji Kylian Mbappe kutoa maoni kuhusu kiongozi wa zamani wa China, Mao Zedong.

Mourinho amesema kutoa kauli zinazoweza kuudhi ni moja ya “hatari za dunia ya sasa”, lakini akamsifu Mbappe kwa kuomba msamaha haraka, akisema alionyesha uwajibikaji na “ustaarabu wa kweli”.

Mbappe aliomba msamaha baada ya kusema kuwa picha ya kuchekesha iliyomfurahisha zaidi ilikuwa ile iliyounganisha uso wake na picha ya “dikteta wa China” aliyefanana na Mao Zedong, aliyefariki mwaka 1976.

MOU 03

Mourinho aliulizwa kuhusu suala hilo katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa La Liga dhidi ya Racing Santander uliopangwa kuchezwa leo Jumapili.

“Katika dunia ya sasa, hizo ni hatari zake. Mara nyingi jambo bora unaloweza kufanya ni kunyamaza, kwa sababu kuna hatari katika mambo mengi unayosema au kutoa maoni kuyahusu,” amesema Mourinho.

“Lakini nimemwona akichukua hatua kwa uwajibikaji mkubwa kwa klabu ambayo, katika kiwango hiki, ni ya hadhi ya juu kabisa. Kwa upande wetu, hilo ndilo la kusema. Hakuna kingine cha kufanya.”

MOU 01

Mbappe, ambaye wakati mwingine huitwa “dikteta” kutokana na ushawishi wake mkubwa katika soka, alikuwa akizungumzia jina hilo la utani katika kipindi cha mazungumzo cha Ufaransa, The Bridge, alipoulizwa kuhusu picha za kuchekesha zinazomfurahisha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema picha iliyomchekesha zaidi ilikuwa video ya mtu ambaye alidhani ni dikteta wa China. Kisha kipindi kikaonyesha picha iliyounganisha uso wa Mbappe na taswira inayofanana na Mao.

Kipande hicho cha mazungumzo kilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii nchini China na maeneo mengine duniani, na kusababisha baadhi ya kampuni za China kusitisha ushirikiano wao na Mbappe.

MOU 02

Jumanne, mshambuliaji huyo wa Real Madrid alitoa taarifa ya kuomba msamaha kwa kauli aliyoieleza kuwa “isiyofikiriwa vizuri”. Amesema sasa anaelewa kuwa iliumiza watu wengi nchini China na katika jamii za Wachina duniani.

Mourinho, ambaye aliiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga msimu wa 2011/12 katika kipindi chake cha kwanza klabuni hapo, aliulizwa pia kama ana wasiwasi kuhusu video za bandia zinazotengenezwa kwa akili bandia na kuonyesha kauli ambazo yeye au Mbappe hawakusema.

“Sina wasiwasi,” amesema. “Klabu yangu ni Real Madrid, na mchezaji wangu ni Kylian Mbappe.

“Real Madrid na Kylian Mbappe wameonyesha hadhi kwa kuchukua hatua mara moja, na ninahisi nimewakilishwa vizuri sana na wote wawili.”