Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kashfa ya Mbappe majanga kwa Real, La Liga

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, klabu hiyo inaweza kupoteza sehemu ya mapato baada ya kampuni kadhaa za China kusitisha mikataba ya kibiashara na Mbappe kufuatia kauli zake kuhusu picha ya utani iliyomhusisha aliyekuwa kiongozi wa zamani wa China, Mao Zedong.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid inakabiliwa na changamoto ya kibiashara kufuatia utata uliohusisha mshambuliaji wake Kylian Mbappe nchini China, hali inayoweza kuathiri mapato ya klabu hiyo kupitia mikataba ya udhamini, mauzo ya jezi na haki za matumizi ya picha za wachezaji.

Mafanikio ya kibiashara ya Madrid yanategemea kwa kiasi kikubwa umaarufu wake duniani, unaochangiwa na nyota kama Mbappe, ambao huisaidia klabu kupata mapato makubwa kupitia udhamini, bidhaa za klabu na mikataba ya matumizi ya picha zao.

Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, klabu hiyo inaweza kupoteza sehemu ya mapato baada ya kampuni kadhaa za China kusitisha mikataba ya kibiashara na Mbappe kufuatia kauli zake kuhusu picha ya utani iliyomhusisha aliyekuwa kiongozi wa zamani wa China, Mao Zedong.

MBAP 01

Kampuni za Dongpeng Beverage, Mengniu na Milkground zimeripotiwa kusitisha ushirikiano wao na mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Mbappe anaripotiwa kupata takribani euro30 milioni kwa mwaka kupitia mikataba ya matangazo, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye thamani kubwa kibiashara katika soka la dunia.

Kwa kawaida, Real Madrid hupata asilimia 50 ya mapato ya haki za matumizi ya picha za wachezaji wake, ingawa Mbappe alifanikisha makubaliano yanayomruhusu kubaki na sehemu kubwa zaidi ya mapato hayo.

MBAP 02

Hata hivyo, Madrid bado inanufaika kifedha kupitia baadhi ya mikataba ya kibiashara inayomhusisha mshambuliaji huyo, hivyo kusitishwa kwa udhamini wake kunaweza pia kuathiri mapato ya klabu.

Kiasi halisi cha fedha ambacho Madrid inaweza kupoteza bado hakijafahamika, kwa kuwa thamani ya mikataba iliyositishwa haijawekwa wazi.

Mbali na mikataba ya udhamini, klabu hiyo pia ina wasiwasi kuhusu mauzo ya jezi zake nchini China, ambayo ni miongoni mwa masoko muhimu ya bidhaa za Madrid.

MBAP 03

Ripoti hiyo inakadiria kuwa takribani asilimia 15 ya jezi zote zinazouzwa na klabu hiyo duniani zinanunuliwa nchini China. Jezi ya Mbappe yenye namba 10 mgongoni pia imetajwa kuwa ndiyo inayouzwa zaidi kwa sasa.

Iwapo hasira za mashabiki wa China dhidi ya Mbappe zitaendelea, mahitaji ya jezi na bidhaa nyingine za Real Madrid yanaweza kupungua, na kuongeza athari za kifedha kwa klabu hiyo.

Wakati huohuo, shirika la utangazaji la China, CCTV, limesitisha matangazo ya Ligi Kuu ya Hispania, licha ya Mbappe tayari kuomba radhi kuhusu kauli zake. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, CCTV haijaona ombi hilo la radhi kuwa sababu ya kubadili msimamo wake.

MBAP 04

Utata huo umeendelea kukua na sasa rais wa La Liga, Javier Tebas, anashiriki katika mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Kwa sasa, kipaumbele cha La Liga na Real Madrid ni kurejesha uhusiano mzuri na soko la China na kuzuia athari zaidi za kibiashara.

Hata hivyo, bado haijafahamika ni kwa muda gani mgogoro huo utaendelea na ukubwa wa athari zake kwa mapato ya klabu hiyo yenye mashabiki wengi duniani.