Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnazi wa Arsenal amwambia Arteta “Vunja benki bana!”

Arteta Pict

Muktasari:

  • Huo ndio mtazamo wa Piers Morgan, ambaye anataka klabu yake izame mfukoni dirisha hili la uhamisho kunasa mchezaji ambaye atakuja kuleta ahueni kwenye kikosi baada ya sasa mambo kuonekana kuwa magumu huko London Kaskazini.

LONDON, ENGLAND: SHABIKI kindakindani wa Arsenal, mtu maarufu, Piers Morgan amemwambia kocha Mikel Arteta anapaswa kuwaambia mabosi wavunje benki kumsajili straika wa Newcastle United, Alexander Isak kwa sababu Kai Havertz hana kitu atafanya tena kuifikisha timu hiyo inapotaka kufika.

Huo ndio mtazamo wa Piers Morgan, ambaye anataka klabu yake izame mfukoni dirisha hili la uhamisho kunasa mchezaji ambaye atakuja kuleta ahueni kwenye kikosi baada ya sasa mambo kuonekana kuwa magumu huko London Kaskazini.

Sare dhidi ya Brighton kwenye Ligi Kuu England wiki iliyopita iliifanya timu hiyo kuachwa nyuma pointi sita na vinara Liverpool, kabla hawajachapwa na Newcastle United 2-0 kwenye nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Ligi, wakisubiri mechi ya marudiano.

Mambo yamezidi kuwa mabaya kwenye kikosi hicho baada ya Arsenal kushindwa kuishinda Manchester United iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kwenye mchezo wa Kombe la FA, Jumapili iliyopita, ambapo Havertz alikosa nafasi kibao za kuifungia mabao e na hivyo kupoteza taji la Kombe la FA kwa msimu mwingine. Mchezo ujao ni dhidi ya mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur kwenye Ligi Kuu England.

Kutokana na Bukayo Saka kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu huku kukiwa na uwezekano wa kumkosa Gabriel Jesus, bila shaka Arsenal itakuwa na udhaifu mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji na hilo ndilo linalomtia shaka shabiki wa kutupwa wa Arsenal, Mogan.

Akizungumza kwenye kipindi cha talkSPORT Breakfast, Morgan alisema: “Mara ngapi nimekuja kwenye shoo yako kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita tangu Pierre-Emerick Aubameyang alipofunguliwa mlango wa kutokea?

“Alikuwa straika wa kiwango cha dunia na alikuwa akiifungia Arsenal mabao ya rekodi. Sawa, Arteta hakumtaka, sawa, kwa hiyo ni nani aliyekuja kuchukua mikoba yake? Ukweli ni kwamba najaribu kulisema hili kwa upole tunahitaji kusajili mshambuliaji anayejielewa. Lakini, zitafika siku za upole utakwisha.

“Tunahitaji straika mwenye njaa! Mshambuliaji asilia!”

Mchezaji mmoja ambaye Morgan anaamini atakwenda kufiti vyema kwenye kikosi hicho ni staa wa Newcastle United, Isak, ambaye amefunga mabao 15 katika michuano yote msimu huu, ikiwamo mabao 10 aliyofunga kwenye mechi tisa za mwisho.

Alipoulizwa imsajili nani, Morgan alijibu: “Ningechukua kiroba changu cha pesa na kwenda nazo hadi Newcastle na ningevunja benki kumsajili Alexander Isak. Pauni 100 milioni, Pauni 120 milioni, Pauni 140 milioni, Pauni 150 milioni  – sijali. Nitatafuta wachezaji kutoka kwenye mabeki wetu 87 tuliowasajili kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwauza ili kupata pesa za kuiweka timu salama kwenye ishu ya usawa wa mapato na matumizi. Kwa namna tunavyocheza, nafasi tunazotengeneza – unajua ni mashuti mangapi tumepiga hii wiki? 49.

“Unajua ni mabao mangapi tumefunga? Moja. Unajua ni nani aliyefunga? Gabriel, beki wa kati.

“Kama hilo halikuambii kitu, sijui kitu gani kitakwambia. Hatuna straika anayeeleweka, mmoja wa wachezaji wetu tuliowafanya mastraika ni Gabriel Jesus, ambaye kwa sasa kinachoonekana atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima kutokana na kuumia. Namwonea huruma.

“Hili wazo la kwamba Kai Havertz atakuwa mtu wa kutusaidia kushinda ubingwa ni ujinga na kila shabiki wa Arsenal anafahamu hilo. Kama ni hivyo, Mikel Arteta kwanini hajui? Kwanini anaweka imani mkubwa kwa mchezaji huyo ambaye ni mzuri ila sio namba 9. Siyo straika.”

Alipoulizwa kuhusu Isak, Morgan aliongeza: “Kama unataka kushinda mataji makubwa na kuwa na timu hatari kwa kufunga mabao nenda kasajili wachezaji bora. Na kwa sasa, Isak ni straika bora Ulaya. Arsenal, vunjeni hiyo benki yenu bana!”